Habari za Punde

Nafasi za kazi Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI


Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kama ifuatavyo:-

1. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya katika fani ya Uchumi au Planning’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2. Afisa Sera Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya katika fani ya Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3. Mtengenezaji wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ICT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Mhandisi wa Kompyuta Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Compyuter Engineering’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

5. Mhandisi wa Mawasiliano Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Telecommunication Engineering’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

6. Msimamizi Mtandao Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Information System and Network Engineering’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar






Jinsi ya Kuomba:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 -ZANZIBAR.

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .

g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 10 Agosti, 2018 wakati wa saa za kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.