Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Falme za kiarabu (UAE) inatarajia kufungua
Ubalozi wake mdogo Zanzibar kabla ya kumalizika Mwaka
2018 ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha mahusiano ya
kidugu katika nchi hizo.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa
Kiamataifa wa UAE, Reem Ibrahim Alhashimy
alipozungumza na Wanahabari mara baada ya kumalizika
kwa mkutano wa majadiliano kati ya Viongozi wa Serikali ya
Zanzibar na UAE ukumbi wa Hotel ya Park Hyyat Mjini
Zanzibar.
Amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo kutazidisha
mashirikiano yaliyopo na kuongeza kasi ya utekelezaji wa
yale yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Reem amesema madhumuni ya kuja Zanzibar ni
kuihakikishia Serikali na Wananchi wa Zanzibar kwamba
UAE ipo tayari kutekeleza yale yaliyoahidiwa katika Ziara ya
Dkt Shein iliyofanyika nchini humo mwanzoni mwa mwaka
huu.
Amesema kwa muda mrefu Wananchi wa UEA wamekuwa
wakitembelea Zanzibar na kuwekeza katika maeneo mbali
mbali kutokana na mahusiano mema yaliyojengeka miaka
mingi.
“Binafsi sio mara ya kwanza kuja Zanzibar nimekuwa
nikitembelea kutokana na uzuri wa Zanzibar na watu wake
na hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kushirikiana katika
mambo yetu” alisema Reem
Sekta muhimu ambazo Serikali ya ya UAE imeonesha nia ya
kuisaidia Zanzibar ni pamoja na Sekta ya Afya, Kilimo na
Miundombinu.
Hata hivyo hakuainisha zaidi ni eneo gani kati ya Bandari na
Uwanja wa ndege ambalo UAE wataweza kuisaidia Zanzibar.
Kwa upande wake Wanziri wa Nchi Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu
amesema ziara hiyo imefungua matumaini makubwa kwa
Zanzibar na kwamba itasaidia Zanzibar kujikwamua
kiuchumi.
Amesema mbali na miradi iliyoombwa na Serikali ya
Mapinduzi kwa UAE nchi hiyo pia ipo tayari kuisaidia
Zanzibar katika miradi mingine ya ziada, ikiwemo uwezeshaji
wa Vijana ili kukabiliana na tatizo la ajira.
Timu hiyo ya Wataalam iliwasili jana na kufanya Mikutano
mbalimbali ya majadiliano na Viongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
mbalimbali zilizotolewa katika ziara ya Dkt. Shein
aliyoifanya January mwaka huu katika Falme za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment