Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Yamwaga Neema Kwa Wanafunzi Wa Kidatu Cha Sita Zanzibar Kutoa Zawadi ya Shilingi Milioni Moja Kwa Mwanafunzi Atakayepata Alama ya A.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd. (PBZ) Ndg. Juma Ameir Hafidh akisisitiza jambo wakati akitowa nasaha zake na kuwapongeza Wanafunzi wa Kidatu cha Sita 96 wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kwa kufanya vizuri mitihani yao ya Taifa na kupata Division I.kushoto Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Light Fuondation  Salim Mussa, Mkurugenzi wa Rom Sulution Ltd,Bi. Viorica Enescu na Mtangazaji na Msanii Salama Jabir.Wadau wa kuhamasisha Elimu Zanzibar.     

Amesema tayari walishatowa zawadi ya fedha taslim kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita waliofanya vizuri na kupata Alama 3 za A na kuwazawadia shilingi milioni Tatu kila mmoja Wanafunzi hao waliopata Division I.3 Biubwa Khamis Ussi wa Skuli ya Sekondari ya SOS na Fahad Rashid Salum kutoka Skuli ya Sekondari ya Lumumba Zanzibar. 

Ametoa ahadi hiyo kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita wa mwaka wa masomo 2018/2019 wakifanya vizuri na kupata Alama ya A atainunua kila moja kwa Shilingi Milioni Moja, ahadi hiyo ameitowa wakati wa hafla ya kukabidhiwa Komputa Wanafunzi 96 wa Skuli 17 za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Kisonge.

Komputa hizo zimetolewa na Kampuni ya Rom Sulution Ltd kupitia ahadi iliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, kuwaahidi wafunzi hao watakaofanya vizuri mitihani yao ya Taifa atawazawadia Laptop kila mmoja na kutimiza ahidi hiyo katika viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.