Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Azindua Kikosi Kazi Cha Kutatua Changamoto za Viumbe Wageni I/Vivamizi Nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa  Uzinduzi wa Kikosi cha kutatua changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi John Malongo akiwatambulisha Wajumbe 18 wa Kikosi Kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi hicho kilichozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini mara baada ya uzinduzi wa Kikosi kazi hicho uliofanyika kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.