Habari za Punde

MlipukoMkubwa wa Kujitoa Muhanga Walikumba Jiji la Mogadishi

Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba watokea Nchini Mogadishu.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ameshambulia ofisi ya serikali kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kusababisha shule iliyokuwa karibu kuporomoka, kwa mujibu wa polisi.
Shambulizi hilo la kutumia gari kwenye wilaya ya Howlwadag liliwaua wanajeshi watatu na kujeruhiwa watu 14 wakiwemo watoto 6.
Mlipuko huo pia uliharibu nyumba zilizo karibu na kung'oa paa la msikiti mmoja.
Kundi la wanamgambo wa al-Shabab ambalo limekuwa likiendesha mashambulizi kwa zaidi ya miaka 10 lilisema liliendesha shambulizi hilo.

Wanajeshi watatu waliuawa walipolisimamisha gari lililokuwa limejazwa milipuko kuingia kwenye makao ya serikali.
Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba Mogadishu.
Raqiya Mahamed Ali, ambaye alikuwa ndani ya makao hayo alisema: "Tulikuwa tukiendelea na shughuli zetu wakati mlipuko ulitokea.
"Nilijificha chini ya meza. kulikuwa na milio mingi ya risasi kwenye lango...wakati nilitoka nje, niliona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa na wengine wakiwa wamekufa." aliiambia Reuters.
Somalia imekumbwa na ghasia tangu mwaka 1991 wakati serikali ya kijeshi ilipinduliwa.
Kupindiuliwa kwa Mohamed Siad Barre kulisababisha miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wababe wa kivita na sehemu zingine mbili - za Somalilad na Puntland zilijitenga kutoka Somalia.
Sehemu kubwa ya nchi imekuwa kwenye vita.
Wananchi Nchini Mogadishu wakiwa katika eneo lililoshambulia katika mji huo likikwa limeharibiwa na mripuko huo, mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga walikumba jiji la Mogadishu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.