Habari za Punde

Mohamed Salah: Je anakabiliwa na 'ukame' wa mabao?


Mohamed Salah hajapata bao jingine tangu alipofunga dhidi ya Brighton wiki nne zilizopita.
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa klabu hiyo haitarajii kwamba Mohamed Salah atarejelea ufungaji wake wa mabao kama msimu uliopita na kufanya mzaha kwamba mfungaji huyo anakabiliwa na 'ukame'
Salah ambaye ni raia wa Misri , 26, aliifungia Liverpool mabao 44 msimu uliopita na alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi katika ligi ya Uingereza msimu huo.
Amefunga mara mbili katika mechi sita wakati huu licha ya kuwa na bao moja zaidi wakati kama huu katika kampeni ya msimu wa 2017-18.
"hakuna anayekumbuka alivyoanza msimu uliopita'', alisema Klopp.
Salah aliifungia Liverpool bao la kwanza msimu huu dhidi ya Westa Ham mnamo mwezi Agosti, lakini hajapata bao jingine tangu alipofunga dhidi ya Brighton wiki nne zilizopita.
''Wow, huo ni ukame'', alisema Klopp ambaye timu yake inacheza dhidi ya Southampton siku ya Jumamosi.
''Sio tatizo kubwa. Alipoulizwa iwapo watu wangefaa kutarajia kiwango kama kile cha msimu uliopita kutoka kwa Salah , mkufunzi huyo alisema: Ndio kila mtu anatarajia hilo. ni wazi kabisa.
''Hatutarajii kiwango kama kile lakini tunataraji kwamba atakuwa akifunga mara kwa mara''
Liverpool imeshinda mechi zake tano za kwanza na iko ya pili katika jedwali wakiwa sawa kwa pointi na Chelsea , na Klopp anasema kuwa Salah anasalia kuwa tisho kwa upinzani.
''Katika ulinzi , katika mechi mbili zilizopita alicheza vizuri sana'', aliongezea. ''Yuko tayari kuichezea timu katika wakati huu''.
Ni swala la kawaida kwa washambuliaji kwamba wanakuwa na wakati ambapo hawapati mabao. lakini yeye bado ni tishio, amecheza vizuri mechi zote na yuko katika hali nzuri.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.