Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda Aelezea Tukio la Kutekwa Kwa MO DEWJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza akiwa eneo la tukio ambalo leo October 11, 2018 Mfanyabiashara maarufu nchini MO Dewji ametekwa akiwa anaingia Gym alfajiri.

Amesema tayari upekuzi umeshaanza katika maeneo yote muhimu hasa kwenye hoteli, nyumba za wageni, mipakani na kwenye viwanja vya ndege kuhakikisha jeshi linanasa mtandao wa watuhumiwa waliohusika na utekaji huo

RC Makonda amefafanua kuwa miongoni mwa watekaji nyara, wapo wazungu wawili, hali inayoonyesha kuwa tukio hili limefanywa na wenyeji kwa kushirikisha na raia hao wa kigeni.

Amesema baadhi ya walinzi na wahudumu wa Gym ya Colosseum wamekamatwa ili kulisaidia jeshi la polisi maana wao ndo wanajua ni gari gani ilifika pale, ilikuwa na watu gani na walikaa muda gani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.