Habari za Punde

Aliyemuokoa mwanamke kisimani akabidhiwa hati ya ushujaa




Na. Raya Hamad


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Kichupa amemkabidhi  Hati  ya ushujaa Mohamed Haji Mohamed aliyemuokoa bi Mariam Hassan  Vuai kutoka kisimani. 


Akiwa amefuatana na wajumbe  wa Kamati  ya siasa ya mkoa wa kusini  mwakilishi  wa jimbo  la makunduchi Mwalimu Haroun Ali Suleiman na viongozi wa jimbo Amesema chama kimeguswa na tukio hilo la ujasiri lililofanywa  na  Mohamed la kuamua kujitolea maisha yake kwa kumuokoa mwenzake. 

 Kichupa amesema hivyo Chama cha mapinduzi Mkoa wa kusini Unguja kwa niaba wa wanachama wa ccm wameona ipo haja ya kuthamini juhudi alizofanya Mohamed kabla ya kusubiri kikosi cha uokozi ambacho kutokana maazingira ya bi mariam  kuingia kisimani wangeweza kufika na kuopoa maiti. 

Mapema mwalimu HarounAli Suleiman alitoa salaam  za pongezi rais  wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein kuwa anathamini juhudi zilizofanywa na ndugu Mohamed katika kuokoa uhai wa bi Mariam.

Ndugu Mohamed akielezea tukio hilo amesema alikuwa maskani akicheza keram akaja itwa kwa na kujulishwa kuwa mtu kutumbukia kisimani mtaa wa kiongozi jimbo la la makunduchi  hivyo aliamua kujitolea kutoa taarifa polisi.

Baada kuja polisi na kukamilisha taratibu za kiusalama aliingia kisimani na kufanikiwa kupiga mbizi na kumfunga bi Mariam kamba ya kiuno na kujifunga mwenyewe kwa kumpakata na kuwatumia waliopo juu kwa  kuwavuta na hatimae kuweza kumfikisha juu akiwa salama. 

Aidha ujumbe  huo kwa pamoja ulifika nyumbani kwa mama yake bi Mariam Hassan Vuai  kwa ajili ya kumpa pole yeye  na familia yake.
Bi Mariam alijitumbukiza kisimani kutokana na tatizo la ugonjwa wa akili katika shehia ya kiongoni jimbo la makumbusho tarehe 9 mwezi wa 10 mwaka huu 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.