Habari za Punde

Kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Yatembelea Vikundi Vya Vijana Kisiwani Pemba.

Mkalimani wa lugha za alama Zanzibar Amina Abeid, akimtafsiria Mwakilishi wa viti maalumu Zaina Abdalla, wakati kamati yake wa Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ilipokua ikikagua kikundi cha ufugaji wa samaki Sizini Wilaya ya Micheweni.
Katibu wa Kikundi cha Umoja na Mshikamano Sizini kinachojishuhulisha na ufugaji wa Samaki Ali Omar Hamad, akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, wakati walipotembelea kikundi chao na kuangalia ufugaji wa samaki
WAJUMBE wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakitoka kukagua ufugaji wa samaki katika mabwawa ya baraza la Vijana Wilaya ya Micheweni huko Sizini Wilaya ya Micheweni
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.