Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Azungumza na Waandishi wa Habari.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar, kuhusu kutunza amani wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2019.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza    kuhusu kutunza amani wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2019 huko  Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar.


Na Mwashungi Tahir.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wananchi wa Mkoa wa Mjini kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa kiwanja cha Mao Tse Tung  likiwa ni tukio la Historia kwa hapa Zanzibar na linatarajiwa kufanyika tarehe 3/1/2019.
Akizungumza na waandishi wa habari  huko Ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumzia mafanikio yaliyopatikanwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi  kwa Mwaka 2018  na kuukaribisha mwaka 2019  ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ikiwa ni muendelezo kila ifikapo mwisho wa mwaka.
Alisema uzinduzi wa Mao Tse Tung ni tukio la pili la Historia kwa Mkoa wa Mjini Magharibi  ambapo tukio la mwanzo la  historia ni Ufunguzi wa Uwanja wa Michezo Amani, na kufunguliwa na Marehemu Mzee Amani Karume katika Mkoa huo.
Hivyo alisema miradi mengine 13  ni pamoja na ufunguzi  wa Skuli ya Bwefum, uzinduzi wa bara bara kutoka Fuoni mambo sasa  na kwa mabata hadi kinuni , kituo maalum cha DNA ni mashine ya kupimia minasaba kwa Mkemia Mkuu  na  kuweka jiwe la msingi ZBS  pia kutakuwa na makongamano .
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mambo mengi ya maendeleo nchini kwa lengo la kuwataka wananchi wake waishi kwa amani na utulivu.
Pia amewaomba wananchi washerehekee  mwaka mpya kwa taratibu za jeshi la ulinzi na usalama   kwa amani bila ya uharibifu wa barabara, waepuke kuendesha vyombo kwa mwendo wa kasi wakiwa wamelewa kwani kufanya hivyo kutaweza kuwasababishia ajali na kuweza kupata ulemavu au kupoteza maisha .
“Nawaomba wale wenye kawaida ya kuzunguka katika round about kwa fujo waache mara moja washerehekee mwaka mpya kwa amani na utulivu kwani sehemu zote za Mkoa huu tumeweka jeshi la ulinzi na usalama kwa lengo la kutaka wazanzibariA wote wawe katika hali ya amani”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha akizungumzia mikakati ya mwaka 2019 kuondoa kero kwa wananchi , shughuli za maendeleo za Serikali na pia kutatua changamoto kwa  wananchi wake ikiwemo   madada poa  kaka poa na omba omba  kuhakikisha wanaondoka kabisa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.