Habari za Punde

*GAVANA SHILATU ATAKA UMOJA UJENZI MRADI WA MAENDELEO*Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ametaka umoja, ushirikiano na upendo wakati wa usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuleta tija, ubora na ufanisi wa mradi.
Gavana Shilatu ameyasema hayo Leo Jumapili Januari 6, 2019 wakati alipotembelea mradi ujenzi wa soko katika Kijiji Cha Shangani kilichopo kata ya Michenjele ambapo ameagiza Serikali ya Kijiji, Kamati ya ujenzi na Mkandarasi kuwa kitu kimoja ili mradi wa ujenzi ukamilike kwa wakati na kwa viwango vyenye ubora.
"Mradi unajengwa vizuri. Ongezeni na imarisheni umoja, upendo na mshikamano wenu, nawasihi sana. Wekeni pembeni tofauti zenu Kama zipo na msimamie vyema zaidi mradi wa ujenzi huu wa soko kiukamilifu, simamieni ipasavyo mradi huu, penye kasoro mparekebishe. Sote kwa pamoja tulijenge Taifa letu kwa Umoja, Upendo na Mshikamano."* alisema Gavana Shilatu.
Katika ziara hiyo ya kukagua mradi wa ujenzi huo wa soko, Gavana Shilatu aliambatana na Diwani Kata ya Michenjele, Mtendaji kata ya Michenjele, Serikali ya Kijiji Cha Shangani pamoja na Kamati ya ujenzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.