Habari za Punde

Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ( IJA) Yatoa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo ZURA

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Jaji,Dkt.Paul Kihwelo ambaye pia ni mratibu wa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kanuni na mbinu za usuluhishi wajumbe wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za maji na Nishati Zanzibar (ZURA)  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama wilayani Lushoto yenye lengo la kuwajengea uwezo waweze kufanya kazi za mamlaka hiyo kwa waledi ambapo yaliyofanyika chuoni hapo
 Mwezeshaji Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
 Mwezeshaji Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani wa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kanuni na mbinu za usuluhishi wajumbe wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar (ZURA) katikati akiwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Jaji John Mroso kulia na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Rose Temba ambaye pia ndie mwanzilishi wa kituo cha Usuluhushi akihudumu kama Jaji Mfawidhi wa kituo hicho wakiwa kwenye mafunzo hayo
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa umakini
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakijitambulisha
Mwezeshaji  wa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kanuni na mbinu za usuluhishi wajumbe wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar (ZURA)Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani katikati akiwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Jaji John Mroso kulia na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Rose Temba ambaye pia ndie mwanzilishi wa kituo cha Usuluhushi akihudumu kama Jaji Mfawidhi wa kituo hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki kulia wa kwanza waliosimama ni Jaji Dkt Paul Kihwelo ambaye pia ni Mkuu wa chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA)



CHUO cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) leo wamefungua mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kanuni na mbinu za usuluhishi wajumbe wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar (ZURA).

Mafunzo hayo ya siku tano yaliyoanza leo yanafanyika kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama wilayani Lushoto mkoani Tanga yakiratibiwa na Jaji Dkt Paul Kihwelo ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Jaji Dkt Kihwelo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi na viongozi wa ZURA ili waweze kufanya kazi za mamlaka yao kwa waledi mkubwa kuliko ilivyokuwa awali.

“Ni matumaini yetu kwamba baada ya mafunzo watakuwa wanafahamu zaidi kanuni na mbinu mbalimbali za usuluhishi katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kuzifanya kwa waledi”Alisema Jaji Kihwelo.

Aidha alisema pia pamoja naye chuo hicho kimeandaa wakufunzi waliobobea katika eneo la usuluhishi ili kuipa ZURA kile wanachostahili ili waweze kufahamu mbinu mbalimbali za usuluhishi kwenye maeneo yao.

Awali akizungumza Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani alisema jambo muhimu kwenye usuluhishi mafanikio yake sio nani kashinda na nani kashindwa.

Alisema kama kesi inayokwenda mahakamani bali ni kurudisha uhusiano mwema kati ya pande mbili zilizopo kwenye mgogoro na wao wenyewe kuweza kutatua mgogoro wao na sio kumuachi mtu wa nje pamoja na kwamba ni mtu huru jaji au hakimu kuweza kusuluhisha.

Alisema pia kwa sababu kuna umuhimu wa mgogoro kusuluhishwa na wenye mgogoro wenyewe na sio mtu wa nje ndio tofauti kubwa pili ni kwamba ili  kusuluhisha ufanikiwa lazima wale wenye mgogoro waingie kwenye usuluhushi wakiwa tayari kutoa na kupokea kwa sababu ukiingia huko
wanaoshinda ,wanaokosa wote lakini mahakamani ana shinda mmoja anakosa mwengine.

Aidha alisema kwenye usuluhishi wote waliopo kwenye mgogoro ni washindi wote kila mtu anapata na katoa lazima utoe na upokee pia ni jambo jingine muhimu kwa watanzania na Zanzibar njia moja ya kisheria ya kutatua migogoro ni kupitia mahakama.

Jaji Mkuu Mstaafu huyo alisema pia sheria za nchi zetu mbili pamoja na katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 107 (a) ibara ndogo2(d) inamtaka moja katika msingi wa utoaji haki ni kutatua migogoro kwa njia mbadala na ndio maana kwenye mashauri ya kazi kuna njia
mbadala za kwenda kwenye Mahakama za usuluhishi (CMA).

Alisema pia kwenye masuala la talaka ndoa kabla hujaletewa mashauri mahakamani lazima uende kwenye bodi ya usuluhishi na ni njia mbadala ya kuweza kutatua migogoro hiyo kwa njia ya haki mtu kupata haki kwa sababu haki haipatikani mahakamani pekee.

Naye kwa upande wake Mwanzilishi wa kituo cha Usuluhishi Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ,Jaji Rose Temba alisema kituo hicho kilianzishwa  ramsi kwa ajili ya mashauri ya madai yanapopelekwa mahamakani kwa kutambua kwamba sheria inataka usuluhi ufanyike kabla ya shauri
halijaingia kusikilizwa rasmi .

Alisema kutokana na hilo uongozi wa mahakama ukaona ni bora uanzishe kituo hicho ili kuwe na wataalamu ambao ni majaji watakaokuwa na kazi yao ya kila siku ni kufanya usuluhishi na hiyo ilitokana na ukweli kwamba majaji waliopo kwenye vituo vyao wanafanya kazi nyingi kwa
wakati mmoja.

Alisema unakuta wanfanya kazi za usuluhishi na kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi wakati mmoja hivyo wakaona ni jambo jema kama kutakuwa na kituo ambacho kitakuwa ni kupoeka mashauri yaliyoiva kwa ajili ya kufanya usuluhishi.

Hata hivyo alisema tokea kituo hicho kimeanzishwa kumekuwa na mafanikio ndani yake maana jaji aliyepo kwenye kituo hicho ana muda wa kutosha kuyasoma majalada na kueleza kiini cha matatizo kabla ya wadawa hawajafika ili kuweza kuendesha mjadala wa masuluhishio.

Naye kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ally Abood Mzee Mjumbe alisema wao wamepata bahati ya kuhudhuria mafunzo hayo ya usuluhishi ambayo ni muhimu kwao kwa kuwawezesha kujua namna ya kuweza kwenda kutatua migogoro inayokuwa ikijitokeza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.