Habari za Punde

Ufunguzi wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Masikini

Mdhamini wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Kisiwani Pemba, Haroub Ali Massoud , akitowa ufafanuzi wa maeneo yanayotarajiwa kufanyiwa utafiti wa mapato na matumizi ya kaya kwa mwaka 2019/2020, huko katika ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake Pemba.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Bi.Mayasa Mahfoudh, akitowa nasaha zake kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya kwa mwaka 2019/2020 na kumkaribisha Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, ili kufunguwa mafunzo kwa Wadadisi hao huko katika kumbi wa Baraza la Mji Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, akifunguwa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa utafifiti wa mapato na matumizi ya kaya (HBS) mwaka 2019/2020 yaliofanyika katika ukumbi wa Baraza la
Mji wa Chake Chake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.