Habari za Punde

Magomeni Waweka Mikakati Kuboresha Mahusiano na Wageni Wao Kutoka Dar es Salaam Wakati wa Tamasha la Pasaka Zanzibar.

Na.Mwandishi Wetu.
Uongozi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar umeahidi kuweka Mikakati madhubuti itakayokuza uhusiano uliopo baina yao na Kata ya Mbagala Kuu na Magomeni kutoka Jijini Dar-es-saalam na kuimarisha uchumi wa Nchi.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Mhe.Jamal Kasim Ali huko Tawi la CCM Meya juu katika usiku wa Faraja uliombata na Sherehe za kuwaaga wageni wao kutoka Mbagala kuu na Kata ya Magomeni Jijini Dar-es-Salaam, walipokuwa katika Tamasha la Pasaka  lililofanyika Zanzibar mwaka huu.
Amesema Mikataba ya waliokubaliana ni ya muda mrefu hivyo ni vyema kukaa pamoja na kuifanyia marekebisho ili kuweza kuendana na wakati uliopo kwa faida ya pande mbili hizo.
Aidha amesema tokea kuanzishwa kwa urafiki huo wamepata mafanikio makubwa Kijamii,Kisiasa na Kiutamaduni jambo ambalo linapaswa kuendelezwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amesema mafanikio yaliopatikana yametokana na Muungano madhubuti wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume hivyo watashirikiana kwa hali na mali katika kuenzi na kuutunza kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.