Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa
la Zimbabwe kabla ya kuweka shada la
maua katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini Zimbabwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa
la Zimbabwe katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini
Zimbabwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo hilo
la makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe.
Mnara wa Kumbukumbu katika eneo la
Makaburi ya Mashujaa wa Zimbabwe kama linavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania
katika kikao na Ujumbe wa nchi ya Zimbambwe kilichokuwa kikiongozwa na Rais wa Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa katika Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe leo tarehe
29/05/2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu Kaburi
la mmoja wa Mashujaa wa Zimbabwe Herbert Wiltshire
Pfumaindi Chitepo ambaye aliuwawa mwezi march 1975. Marehemu Herbert Wiltshire
Pfumaindi Chitepo alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka DPP mweusi wa kwanza Tanganyika na Afrika.
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment