Habari za Punde

KATIBU WA UENEZI NA ITIKADI CCM TAIFA HAMPREY POLEPOLE KUTOA BAJAJI KUMI MKOANI WA IRINGA

Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Hamprey Polepoleakiongea wakati akiwa kwenye ziara ya kimkakati ya siku moja mkoani Iringa
Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Hamprey Polepole  akiongea na madereva bajaji wakati wa kuzindua tawi la bajaji manispaa ya Iringa.
 Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Hamprey Polepole akisoma kibao cha tawi alilolifunga mtaa wa mwembetogwa manispaa ya Iringa.

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Hamprey Polepole ametoa bajaji kumi kwa umoja wa madereva bajaji mkoa wa Iringa ili ziweze kuwasaidia kujikwamua kiuchumiwa tawi hilo mkoani hapa

Polepole alisema kuwa chama cha mapinduzi ni  ni chama kinachofanya kazi kwa vitendo hivyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kuchapa kazi kwa kuwa chama hicho kitatoa bajaji kumi ili ziweze kuwasaidia vijana kujikwamu kiuchumi.

“Nimekuja hapa leo kuja kufungua tawi lenu hili lakini nimesikia risala yenu kuwa kuwa munaitaji bajaji na viwanja,chama hiki sio chama cha porojo tunafanya kazi kwa vitendo sasa mwenyekiti  wa wilaya
hizi kadi usitoe leo zitoe tarehe 20/7 mwaka huu ukiambatanisha na bajaji kumi ili ziwasaidie vijana wetu hawa wanao muunga mkono Rais wetu John Pombe Magufuli”

Alisema kuwa maendeleo ya nchii hii hayana chama hivyo anaamini bajaji walizozitoa zitawabeba watu wote wenye vyama na wasio na vyama hivyo
ni vyema wakatumia bajaji hizo vyema ili ziweze kuwapatia viwanja walivyovihitaji.


“Ndugu zangu mlisema mnahitaji viwanja au kauli kwa tasisi za fedha ili muweze kukopeshwa fedha kwakuwa hamna dhamana sasa hizi bajaji kumi zikawe ni dhamana kwenu ili sasa muweze kufanya kazi na ziwe dhamana kwenu ili muweze kuongeza bajaji nyingine ili sasa vile viwanja mulivyoomba muvipate kwa kutumia bajaji hizi”


Polepole alisema kuwa kwa hamasa aliyoiona na ari ya vijana wa mkoa wa Iringa anaamini mateso na machungu waliyoyapata wanairinga kwa kukosa mwakilishi anayejali na kuishi matatizo ya wanairinga bungeni yamefika mwisho na 2020 wana Iringa  watafanya mapinduzi ya kishindo.

Alisema kuwa wakati wa kufanya siasa za ujanja ujnanja na zisizotekelezeka zimefika mwisho na sasa ni wakati wakufanya siasa za kuishi na kutatuakero za wananchi hivyo wale wote waliofanya siasa ujanjaujanja wajiandae kukabidhi majimbo waliyoazimwa kwa muda.

Awali akisoma risala ya madereva hao katibu wa umoja wa madereva bajaji  hao Salum Gerald  alisema kuwa chama hicho kimefanikiwa kutoa bajaji 36 zenye thamani ya milioni 280 na bajaji gari moja kwa vijana hao ambazo wanazitumia kujiingizia kipato cha kila siku katika Maisha yao

Hata hivyo Gerald alisema kuwa kikundi hicho chenye vijana 800 kinakabiliwa na uhaba wa dhamana na zitaowatesa vijana wengi kupata mikopo na kupata viwanja vilivyo pimwa hivyo ombi lao ni kuomba dhamana ya pesa taslimu au dhamana kwenye tasisi za fedha ili weweze kukopesheka kwa urahisi zaidi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa chama hicho kimejipanga kusikiliza na kutatua kero kwa wanachi wake hivyo kwakuwa wamefanikiwa kuwafikia watu wote hasa wale wa ngazi ya chini wanaamini uchaguzi unaokuja watashinda kwa kishindo

Rubeya alimuhakikishia katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Hamprey Polepole kuwa anafanya kazi vizuri na vijana wote wa manispaa ya Iringa na wanakiunga mkono cha cha mapinduzi kwa asilimia kubwa.

“Saizi Iringa shwari na tumejipanga kuhakikisha tunakomboa jimbo hili ambalo lipo upinzani hivyo vijana hawa ndio nguzo ya chama chetu” alisema Rubeya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.