Habari za Punde

Matukio Katika Picha Uwasilishwaji Mapendekezo Bajeti Kuu ya Serikali

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akionyesha Mkoba unaowakilisha Bajeti Kuu ya Serikali alipowasili katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kuwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Dotto James (kulia) wakifuatiliana Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Katibu Mkuu Kiongozi (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda wakisoma vitabu vya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (hayupo pichani) leo Bungeni jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akipitia kitabu cha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakatiikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango leo Bungeni jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatiliana Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dktt. Phillip Mpango (kulia) mara baada ya kuwasilisha Hotuba yake ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Bungeni jijini Dodoma.
Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji. 
Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. (Picha na: Frank Shija)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.