Habari za Punde

Serikali Yaja na Mfumo Mpya wa Ajira ‘Ajira Portal’ Kukabiliana na Vitendo vya Rushwa na Upendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika (Mb) akisisitiza umuhimu wa Waajiri kutumia mfumo wa TEHAMA katika kutangaza nafasi za ajira ’Ajira Portal’ wakati akizindua mfumo huo ulipo chini ya Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Katibu wa  Sekretarieti ya Ajira katika Umumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi akieleza faida za mfumo mpya wa TEHAMA utakaotumika kuwezesha waombaji wa ajira kutuma maombi yao ya ajira na kupata mrejesho wa maombi yao leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki takribani 140 wa mafunzo kuhusu mfumo mpya wa maombi ya ajira uliozinduliwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika (Mb).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Bi. Riziki Abraham akisisitiza jambo  leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA katika kutangaza nafasi za ajira na kuendesha mchakato wa ajira ’Ajira Portal’ katika Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa maombi ya Kazi leo Jijini Dodoma.Kulia ni Katibu wa  Sekretarieti ya Ajira katika Umumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi na kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.