Na Abdalla Mfaume
Mkuu
Wa Wilaya Ya Kaskazini B Ndugu Rajab Ali Rajab amewataka vijana kuwa wazalendo wa nchi yao na kuachana na tabia ya kujihusisha na mambo
ambayo hayana tija yoyote.
Amesema suala la uzalendo kwa vijana ni suala
muhimu na kusisitiza vijana hao kutokukubali kutumiwa na baadhi ya
wanasiasa kwa ajili ya kutimiza malengo yao ya kupata nafasi za uongozi na baadae
kuwawacha vijana wakiwa hawajui la kufanya bila ya kuwasaidia katika kuwainuwa
kiuchumi.
Kauli hiyo ameitowa wakati akifungua mafunzo
ya siku moja kuhusu umuhimu wa kugombea nafasi za uongozi kwa vijana wa shehiya za bumbwini makoba
,misufini pamoja na mafufuni na kusema uongozi wa wilaya katika kuwasaidia
vijana kujikinga na makundi maovu umeamua kuanzisha miradi mbalimbalil ili
kuwainua vijana hao kiuchumi.
Aidha
Nd:Rajab amewataka vijana wa kike kuacha kukubali kuolewa wakati wakiwa
hwajamaliza skuli kwani kufanya hivyo kutapelekea taifa kukosa
viongozi bora wenye uzalendo na taifa lao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa uvccm wilaya ya mjini bi hudhaima mbarak tahir mkufunzi wa mafunzo hayo ameitaka jamii kuwapa
uhuru vijana hasa wa kike
kugombea nafasi za uongozi pamoja na kuzingatia maadili ya uongozi.
Nao baadhi ya vijana waliopata mafunzo hayo
wamesema mafunzo hayo yamewaelimisha
vizuri na watagombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwatumikia wananchi katika sekta
mbalimbali na wao waepukane kutumiwa kwa
ajili ya watu kupata faida.
No comments:
Post a Comment