Habari za Punde

Vyombo vya habari vitangaze vizuri - Wito

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa Habari,Utalii na Mambo yakale Mahamuod Thibiti Kombo amesema Ustawi wa nchi unaweza kustawi vizuri pale ambapo vyombo vya Habari vinapotangaza Matangazo yake vizuri kwa Wananchi wanao wangalia na kuwasikiliza matangazo yao.
Amsema ustawi huo utapatikana kwa kutoa vipindi vyenye tija vinavyo angalia maslahi ya hichi kwa kuzingatia mila,destueri na tamaduni za wazanzibar ambazo zimekubalika na kufuatwa.
Amesema hali hiyo itwafanya ananchi kuvipenda vipindi vyao na kuviangalia ipasavyo na vyombo hivyo kupata soko kwa watejawao.
Hayo ameyasema leo huko Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kwa watumiaji ya maudhui ya utangazaji katika sherehe ya uzinduzi wa utafiti ulio fanyika Wizarani hapo.
Amesema utafiti ulio fanywa na wataalamu kutoka idara ya takwimu Zanzibar kwa ushirikiano na tume ya Utangazaji Zanzibar ni halihalisi ya vyombo vya Habari vinavyo pendwa zaidi na wananchi kutokana na vipindi vyoa wanavyo vitoa na vyenye maslahi na wao.
Amsema katika utafiti huo ulio aza julai 2017 hadi 2018 kwa upande wa TV  umeonesha wazi kuwa Tv ya Azam ndio ilionekana inapendwa zaidi na ndio yenye watamazaji wengi hapa Zanzibar ya pili ni Star time,ya tatu ni Zanzibar Cabor.
Na kwa upande wa Radio ilionekana Redio inayo sikilizwa zaidi nai ZBC Radio,Swahiba,Asalam na Istikama Radio.
Waziri huyo aliwambia wamiliki wa vyombo vya habari hivi sasa teknolojia ya mawasiliano imekuwa sana hivyo wanahitajika kuwa makini vinginevyo watachwa nyuma.  
Nae katibu mtendaji wa tume ya utangazaji Zanzibar Omar Said Kinimbi alisema kuwa lengo la kufanya utafiti huo nikuangalia jinsi gani jamii iliapokea mabadiliko ya utangazaji kutoka analogi na kwenga dijitali na changamoto zake.
Alisema alisema jumla ya Sheia 65 kutoka Wilaya 11 za Zanzbar shehia 44ni kutoka Unguja na Shehia 21 kutoka pemba ambapo washiriki 2860 walihojiwa wanaume 1408na wanawake walikuwa 1456 walihojiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.