Habari za Punde

Waume waaswa kutumia vyema mafunzo ya maadili ya ndoa kupunguza talaka holela

Na Mwajuma Juma

WANAUME Zanzibar wameshauriwa kutumia Mafunzo ya maadili ya ndoa yanayotolewa na viongozi wa dini kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa ili kupunguza ongezeko la talaka visiwani Zanzibar.

Umetolewa na wanakamati ya Kupambana na vitendo vya udhalilishaji ya wilaya ya Kusini Unguja  walipokuwa wakizungumza na ujumbe wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake juu ya  umuhimu wa wanaume ambao wapo katika mpango wa kuoa kupata Mafunzo kabla ya kuingia katika maisha ya  ndoa.

Walisema kuwa mafunzo ya maadili.ya ndoa  yaliyoanzishwa  na ofisi ya Mufti na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar yana nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la talaka linaloendelea kuongezeka na kuathiri malezi ya watoto.

Hata hivyo walisema kuwa mbali na kuwepo kwa chuo hicho lakini pia na makadhi wanatakiwa kuwaita mapema wanaume hao kuwafahamisha zaidi wiki moja kabla ya kufunga ndoa.

Hivyo Kama ataitwa mapema itakuwa ni jambo zuri.ambalo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wimbi la talaka holela.

Aidha walisema kuwa suala la ndoa linahitaji elimu maalumu ili kuondokana na talaka holela na kuondokana na utekekezaji.

"Mimi naona Bora huyu kijana wa kiume anatakiwa kuitwa wiki moja.kabla ya harusi ili kuelezewa utaratibu wa ndoa kwa sababu siku ile anakuwa anawaza jambo moja.tu.hata ukimwambia anakuwa hazingatii", alisema Mwalimu Zimba Khatibu.

Aidha kwa upande wake Mohammed Rajab Mzale alisema kuwa kuwepo kwa talaka holela kumetokana na kuondoka kwa Utamaduni wa wanandoa kutopeleka kwa babu kwa mtoto wa kiume na Bibi kwa mtoto wa kike kabla ya kufanyika kwa ndoa.

Alisema.kuwa zamani mwanamke anapotaka kuolewa hupelekwa kwa Bibi yake na mwanamme huenda kwa babu yake kwa ajili ya kupatiwa Mafunzo suala ambalo kwa Sasa limetawaliwa na utandawazi.

"Familia zimebadilika Sana kuhusu hilo, siku hizi wapo kwenye utandawazi kwa kuondoa utandawazi zaidi na kuthamini Sana mashoga", alieleza Mzale.

Hata hivyo alisema kuwa hata zile nyimbo zilizokuwa zikiimbwa wakati wa harusi haziimbwi.tena na kusahau Kama zilikuwa na Mafunzo makubwa ndani yake.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.