Habari za Punde

HAFLA YA WAHITIMU NA SEMINA KWA VIONGOZI WA CCM TAWI LA CHINA

Mapema mwezi Juni 2019, Uongozi wa Tawi la CCM China uliandaa na kuwaalika wahitimu/wanachama katika hafla fupi ya kujumuika pamoja na kuwaaga makada waliokuwa wanahitimu masomo yao katika fani na ngazi    mbalimbali za elimu hapa China. Hafla hiyo ilifanyika KITAWI-Tianjin, China, 15/6/2019. Aidha hafla hiyo iliambatana na makabidhiano ya Uwongozi mpya wa Tawi la CCM -CHINA ambao ulifanya chaguzi na kumpitisha Ndugu Salum Mohamed Ramia kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM CHINA.

Siku hiyo hiyo palifanyika Semina ya uongozi haswa katika itikadi. Katibu wa Tawi  Ndugu Yazidi Iddi alimkaribisha Mlezi wa Tawi Ndg. Suleiman Mwenda amabaye alitoa semina ya UONGOZI NA ITIKADI kwa wanachama wote waliohudhuria. 

Tukio jengine lilikuwa kutunukia Hati za utambuzi  kwa viongozi wastaafu wa Tawi, Mashina na Mlezi. Wahitimu wa ngazi na fani mbalimbali wapatao 63 walipokea Hati za pongezi kwa ngazi ya shahada ya Uzamivu 8, kwa shahada ya uzamili 34, kwa shahada ya kwanza 8 na kwa ngazi ya cheti 13.

Mwisho kabisa uongozi wa tawi la CCM China unapenda kutoa shukurani za dhati kabisa na za kipekee kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein(Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi)  na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kwa juhudi za dhati kwa namna wanavyo hakikisha mafanikio makubwa ya kimaendeleo kwa Wananchi wa Tanzania (wakiwemo Diaspora) pamoja na kukuza uhusiano na majirani wa Tanzania na vyama marafiki kikiwemo CPC. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.