Habari za Punde

Mahujaji watarajiwa Zanzibar wapatiwa mafunzo ya kutekeleza ibada ya Hijja

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud akifunguwa Semina ya Mahujaji na Maimamu wa Misikiti katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa dhehebi la Shia Tanzania (TMSC) Shekh Ramadhan Ali akitowa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed wakati wa Semina ya Mahujaji na Maimamu wa Misikiti katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Thaqalain Salum Abbas.
 Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Semina ya Mahujaji na Maimamu wa Misikiti katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Mahujaji watarajiwa Zanzibar wapatiwa mafunzo ya kutekeleza ibada hiyo
 Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.  

Waislamu nchini wametakiwa kutekeleza ibada ya hijja kwakila mmoja  mwenye  uwezo kwani hija ni nguzo muhimu na ni  moja kati ya nguzo tano za Uislamu.

Hayo yameelezwa leo katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud  wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Mahujaji na Maimamu wa Miskiti Zanzibar,yalio andaliwa na jumuiya ya kislamu wa Mashia Tanzania.

Amesema Hija ni jambo  muhimu kwa kila Muislamu mwenyeuwezo wa hali na mali hivyo ipo haja kutekeleza ibada hiyo ya nguzo ya tano katika Uislam.

Amesema iwapo  wenye uwezo wa fedha na kiafya watashindwa kufanya ibada  hiyo wajue wanafanya makosa kwani hija ni nguzo inayo mlazimu Muislamu kuitekeleza kwa vitendo.

Hata hivyo alisema Waislamu wanawajibu wa kufanya hija japo mara moja ndani ya umri wake iwapo amejaliwa kuwa na vigezo vinavyo stahiki ikiwemo uwezo, afya na mali.

Aidha alisema Waislamu wafanye hima kuitekeleza kwani  A
llah akiikubali hija yake na akadumu katika matendo mema mtu huyo malipo yake ni pepo.

“Iwapo Mtu atakubaliwa hija yake na allah na akadumu katika kufanya mema hadi kufa kwake mtu huyo malipo yake ni pepo”alisema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud.

Akielezea zaidi alisema suala la amani katika nchi ni muhimu hivyo ipo haja ya wananchi kuwamakini kuituza  na kuunganisha nguvu zao katika misingi ya dini ili waweze kumtumikia allah kwa wepesi zaidi.

Akizungumzia  vitendo vibaya vya uzalilishaji wa watoto na vijana vinavyo favywa na baadhi ya viongozi wa kidini na viongozi wa kitaifa alisema  ni jambo moja baya sana kwani linawapotezea heshima utu wao na kuwafanya kutoaminika na jamii.

Alisema wapo baadhi ya watu wanatumiwa vibaya kuiharibu jamii yao kwa udhalilishaji wa kingono, kuwabaka watoto kwa kuwalaghai kwa thamani ndogo isio ya kibinadamu.

Vile vile alisema Mkoa wa Mjini magharibi utachukua hatua kali kwa watu hao bila ya kuoneana haya kwa kufuata sheria na miongozo iliopo.

Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Tanzania  Sheikh Ramadhani Ali Mwelekwa alitoa neno la shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud na kuomba ushirikiano wa kitaifa  pale pakitokea  shughuli za kiserikali.

Aidha alisema kuwa Jumuiya yao inatumika kwa kufanya masuala mbali mbali yakiwemo elimu,masuala ya kiafya na maji kwa kutoa huduma kwa jamii ya kitanzania.

Mwenyekiti huyo alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kukubali kuungana nao katika  mafunzo ya mahujaji na maimamu wa misikiti Zanzibar.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.