Habari za Punde

Makamishna wa Mapato wa Nchi za Jumuiya ya Afya Mashariki Wakubaliana Kutumia Teknolojia za Kisasa Kukabiliana na Changamoto za Biashara Haramu.

Na. Hawa Ally.
MAKAMISHNA Wakuu wa Mamlaka ya Mapato kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana na kutiliana saini  maadhimio manane kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika ukusanyaji wa Mapato katika nchini hizo.

Mkutano huo wa 46 wa siku mbili umefanyika hapa visiwani Zanzibar ukiwa na lengo la kubadilishana uzoezfu katika ukusanyaji wa Kodi na Mapato kujadili changamoto pamoja na kupeana mbinu mpya ikiwemo kumtumia mfumo mpya ya kitechnolojia katika kukusanya kodi.

Akiyataja maadhimio nane waliokubaliana kwa pamoja mwenyekiti wa mkutano huo ambae ni Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Edwin Mhede alisema kwa pamoja wamekubaliana kuwa na mikakati shirikishi kwaajili ya kukabiliana na tatizo la uingizaji wa bidhaa kutoka nchini moja hata  nchini nyingine pasipokupitia vituo rasmi vya Fordha. 

Alisema wamekubaliana kutumia technolojia zilizozo za ufanisi na za kisasa katika kukabiliana na changamoto za biashara haramu huku wakati huo huo wakijiandaa kukamilifu kutumia mafanikio yataka nayo  uchumi wa kidigitali kwenye kukusanya ushuru wa Fordha na Kodi za ndani. 

Alisema wamekubaliana Kuwekaza katika mfumo wa pamoja na unaobadilika kulingana na wakati  kwa kufanya uthamini wakati wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchini za jumuiya ya Africa Mashariki ambapo kutakuwa na timu ya kudumu  kufanikisha adhimio hilo. 

Alisema katika kufikia malengo mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana lazima kuongeza ufanisi katika maswala Ya maghala ya kuhifadhia bidhaa mbalimbali  ambazo zinatakuwa zikipita katika mipaka ya nchini hizo pia  kuhimarisha mawasiliano ya Mara kwa Mara hususani katika zile nchini ambazo hazipakani na bahari pamoja na maziwa moja kwa moja. 

Mwenyekiti huyo alisema adhimio la nne  kuongeza ufanisi katika kwenye kusimamia  Kodi ya ongezeko la thamani kupitia vifaa maalum EFD ni Ile mfumo ambayo itasaidia kukusanya Mapato kwa namna ambayo ni rafiki na yenye ukweli itakayopelekea biashara kukuwa. 

Adhimio la tano Kuhimarisha eneo la uchunguzi wa maswala ya kikodi ndani ya  jumuiya kwa mamlaka hizo  kwa kuja na miongozo  mbalimbali na kuhimarisha pamoja na kuitekeleza Ili kukabiliana na changamoto hizi za kiuchunguzi katika eneo la Kodi kwa kuwafundisha wachunguzi Ili wafanye kazi kwa ufanisi na kitaalam watakaofanya kazi hata nje ya mipaka ya nchi zao. 

Aidha adhimio la Sita wamekubaliana kwa pamoja kukabiliana kwa kiasi kikubwa makosa yotokanayo na ukwepaji Kodi ya ongezeko la thamani kwa kuwatangaza watakaobainika kupitia vyombo vya habari vilivyopo ndani ya nchi na vya  jumuiya kwa kuzingatia sheria ya utoaji wa habari.

Adhimio la saba Wamekubaliana lazima watafute mbinu na mikakati ya kuweza kupunguza gharama ya matumizi ya ICT, alisema watatumia ICT lakini kutakuwa na mikataba bora kwa wanaowapa huduma hizo katika eneo la matengenezo Ili wasiwe wanatumia fedha nyingi katika matengenezo ikilinganishwa na kiasi wanachokusanya. 

Hata hivyo adhimio la mwisho la mkutano huo kwa pamoja makamishna hao wa mamlaka za Mapato za nchi za jumuiya ya Africa Mashariki wamekubaliana lazima kuhangaika mbinu mpya  kwenye eneo la Kodi ya makampuni za Kimataifa alisema eneo hilo linahitaji elimu ya hali ya juu na uwezo mkubwa wa kugundua mbinu mbalimbali kwa baadhi ya makampuni yasiyokuwa waaminifu wanazotumia katika kukwepa Kodi. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.