Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Wawakilishi wa Kampuni ya OZUAYDIN Kutoka Nchini Uturuki.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN kutoka Nchini Uturuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz wa Pili kutoka Kulia akimueleza Balozi Seif nia ya Kampuni yake ya kutaka kushirikiana na SMZ katika kuimarisha Uchumi.
Balozi Seif kati kati akiwa katika p[icha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz Kulia yake pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bwana Mehmet Ayain.
 Balozi Seif  Kushoto akiagana na Mwenyekiti wa Kampuni  ya Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN Bwana Mehmet Ayain mara baada ya mazungumzo yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz Kushoto akiagana na Balozi Seif mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Kampuni ya Kimataifa ya inayojishughulisha na Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN kutoka Nchini Uturuki imeonyesha nia ya kutaka kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji wa Ujenzi wa Bandari Mpya Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz akiuongoza Ujumbe wa Viongozi wa Nne wa Kampuni hiyo alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz alisema Kampuni ya OZUAYDIN iliyoasisiwa mnamo Mwaka 1982 imefanya utafiti na kuridhika na harakati za kibiashara zinazofanyika Visiwani Zanzibar ambazo Kampuni yake imeona ipo haja ya kutumia taaluma iliyonayo katika kuongeza nguvu za uwajibikaji katika eneo hilo la Biashara.
Alisema ujenzi wa Bandari mpya ya Kisasa Zanzibar ambayo Kampuni yake ina kila sifa na uwezo wa kujenga miundombinu inaweza kuongeza kasi ya Biashara kwa vile mfumo unaotumiwa katika ujenzi huo unazingatia wakati wa sasa wa sayansi na Teknolojia.
Bibi Ezpa Vildiz Sasmaz alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Mradi huo endapo utafanikiwa katika azma ya Kampuni hiyo Bandari ya Zanzibar inaweza kuwa tegemeo kubwa la Uchumi wake kutokana na kuongezeka kwa harakati za Kibiashara kupitia Mlango huo wa Gati Kiuchumi.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uwepo wa Bandari Mpya Zanzibar kutokana na mabadiliko ya Biashara yaliyopo hivi sasa ni muhimu katika kuchangia mapato ya Taifa.
Balozi Seif alisema Bandari ya Malindi iliyopo hivi sasa inayotegemewa kupokea mizigo mikubwa kutoka Mataifa ya nje hasa Makontena ya bidhaa mbali mbali ni ni ndogo kutokana na msongamano mkubwa wa mizigo inayoteremshwa na meli tofauti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo ya OZUAYDIN kuandika maombi yaliyokamilika ya Mradi huo wa Ujenzi wa Bandari ili Serikali ipate wasaa wa kuupitia na kuona namna itakavyoweza kushirikiana na Kampuni hiyo katika utekekelezaji wake.
Kampuni ya Kimataifa ya inayojishughulisha na Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN imeonyesha nia ya kutakja kuijenga upya Banadari ya Malindi kutokana na harakti zake zinazoonekana kuleta msongamano mkubwa wa bidhaa na mizigo inayoingia na iule inayotoka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.