MWENGE wa Uhuru
ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Pemba, kwa kutumia mchakamchaka mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba ukitokea Mkoani Tanga baada ya
kumaliza ziara yake na kukimbizwa katika Mkoa wa Kusini Pemba
WATENDAJI mbali mbali
kutoka Mkoa wa Tanga wakihudhuria katika hafla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru
katika Mkoa wa Kusini Pemba, mwenge huo uliowasili na kaunza kukimbizwa katika
Wilaya ya Mkoani.
BAADHI ya askari wa
Vikosi vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba, wakiuzingia Mwenge wa Uhuru
baada ya kutua katika ardhi ya Mkoa wa Kusini Pemba
MKUU wa Mkoa wa
Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akimpokea Kiongozi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ali, baada ya kuwasili Kiswani Pemba wakitokea Mkoa
Tanga.
WAKUU wa Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Tanga, wakifuatilia kwa makini makabidhiano ya mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Tanga na Kwenda Mkoa wa Kusini Pemba, hafla iliyofanyika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba
MKUU wa Mkoa wa Tanga
Martin Rubein Shegela (kushoto), akimkabidhi
Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, mara baada
ya kuwasili Kisiwani Pemba ukitokea Mkoa wa Tanga na kuanza kukimbizwa katika
Wilaya ya Mkoani.
MKUU wa Mkoa wa
Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akisoma taarifa ya Mkoa wa huko mara baada
ya kupokea mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Tanga
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla (Kulia),
akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Issa Juma Ali na kuanza
kuukimbiza katika Wilaya hiyo.(Picha na Abdi Suleiman - Pemba)
No comments:
Post a Comment