RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salam za
pongezi Rais wa Jamuhuri ya Misri Abd El Fattah Saeed Hussein Khalil El Sisi,
kwa kuadhimisha miaka 67 ya uhuru wa Taifa hilo.
Katika salamu zake Dk.
Shein alisema kwa niaba yake , wananchi na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anapongeza juhudi zinazochukuliwa na kiongozi
wa Taifa hilo katika kuwaletea maendeleo wananchi wake pamoja na kuimarisha
amani, umoja na mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika, eneo la Mashariki ya kati na duniani kwa ujumla.
Dk. Shein alisema ana
matumaini makubwa kuwa juhudi zinazochukuliwa na kiongozi huyo zitakuwa chachu
katika kuendeleza uhusiano mwema uliopo kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Misri,
kwa faida na maslahi ya wananchi wa nchi mbili hizo.
Aidha, Dk. Shein alitumia
nafasi hiyo kumtakia afya njema na furaha kiongozi huyo pamoja na familia yake
ili aweze kuendeleza amani iliopo na kukuza uchumi wa nchi hiyo.
Taifa la Jamuhuri ya
Misri lilipata uhuru wake mnamo mwaka 1952 baada ya Mapinduzi ya kijeshi
yalioongozwa na Mwanamapinduzi Gamel Abdel Nasser kwa kuuangusha utawala wa
mabavu wa Mfalme Farouk, ambapo Jenerali Mohamed Naguib aliongoza Taifa hilo
kwa mara ya kwanza.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal
Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail:
abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment