Habari za Punde

TCRA KUHAKIKISHA HUDUMA BORA NA ZA UHAKIKA ZA MAWASILIANO KWENYE UJENZI MRADI WA UMEME MTO RUFIJI


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (wapili kushoto) na mmoja wa wajumbe wa bodi, wakiwa kwenye eneo la Mto Rufiji ambako kunajengwa bwawa la kufua umeme wa maji Megawati 2115.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Rufiji
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza kuwepo kwa huduma bora za Mawasiliano katika eneo la Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa maji Mto Rufiji Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, kwenye eneo la Mradi huo Julai 28, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mradi huo mkubwa ni mradi wa kimkakati na TCRA kama msimamizi wa sekta ya Mawasiliano hapa nchini inaamini hakuna uwekezaji unaotendeka bila ya uwepo wa mawasiliano, jamii na watu watakaokuwa wanatekeleza ujenzi wa mradi huo wanapaswa kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote wakiendelea na kazi ya ujenzi.

Ujenzi wa Mradi huo wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Trilioni 6.5 fedha za Serikali, ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli juzi Ijumaa Julai 26, 2019 na utakamilika mwaka 2022 ambapo utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2115.

Akieleza zaidi Mhandisi Kilaba alisema, Shirika la TTCL kama Shirika la Serikali pamoja na watoa huduma wengine ya mawasiliano wanaowajibu wa kuhakikisha mawasiliano yapo na TCRA wajibu wake ni kuhakikisha watoa huduma wanafanya yale wanayopaswa kufanywa.

“Hapa umesema zaidi ya wafanyakazi 6,000 watakuwa kwenye eneo hili, lakini pia hata watakaokuwa wanakuja kufanya utalii kwenye National Park ya Nyerere ni lazima wawe na mawasiliano na mawasiliano ya sasa ni Data, kwahiyo tunachoweza kuagiza hususan TTCL ni kuhakikisha wanaenda kwa kasi kubwa kuweka mawasiliano katika eneo hili na mawasiliano tunayotaka sisi kama wadhibiti ni 4G as Minimum.” Alifafanua Mhandisi Kilaba na kuongeza

“Kwa hiyo 4G siyo isubiri mpaka turbines (mitambo ya kufua umeme)zianze kuzunguka, la hasha, ujumbe tunaowapa kwakweli mwisho wa mwezi wa Nane (Agosti) mwaka huu, watu waanze kupata huduma za 4G katika maeneo haya.” Alisisitiza.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Killimbe alisema Mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa nchi na kwamba TCRA imekuwa ikitembelea miradi mikubwa (Flagship Project), kama vile ujenzi wa SGR, Jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere Terminal III na leo tumekuja hapa kutembelea mradi huu mkubwa wa kimakakati wa bwawa kubwa la kufua umeme wa maji ambao utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi, alifafanua Dkt. Kilimbe.

Alimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa uhakika zaidi kwa kuimarisha miundombonu wezeshi kama vile nishati ya Umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

Nae Mhandsi Mkazi wa ujenzi wa bwawa hilo, Eng.Mushubila Kamuhambwa kutoka kampuni ya TECU, ambayo ni kampuni tanzu ya TANROADS, alisema bwawa hilo litakuwa ni miongoni mwa mabwawa makubwa yaliyotengenzwa na binadamu na litakuwa na urefu wa kilomita 100.

Akieleza faida za bwawa hilo licha ya kuzalisha umeme, pia shughuli za uvuvi wa samaki katika maeneo yatakayoainishwa, ongezeko la Mamba na Viboko ambao wanapatikana kwenye mto Rufiji lakin I pia kuwa kivutio cha utalii.
Hata hivyo alieleza changamoto za mawasiliano ya simu inayowakabili eneo la mradi na kuomba TCRA kuyahimiza makampuni ya simu kuboresha huduma zao.
 "Umbi letu, tunaomba muwasukume hawa wanaotoa huduma za mawasiliano ya simu, kwakweli mawasiliano ni changamoto kubwa sana kwenye eneo hili." Alisisitiza Mhandisi Kamuhambwa.
Baadhi ya wajumbe wa bodi na menejiment ya TCRA wakiwa kandokando ya Mto Rufiji Julai 28, 2019 wakati wa ziara ya kutembeela ujenzi wa Mradi wa umeme wa Mto Rufiji.
 
 Mwenyekiti wa Bodi, TCRA, Dkt. Jones Killimbe akifafanua jambo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi Jmes M. Kilaba, akizungumza mwanzoni mwa ziara hiyo.
 Msafara wa TCRA ukipatiwa maelezo ya utekelezaji wa Mradi.
 Msafara wa TCRA ukiwa eneo la mradi


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.