Habari za Punde

TRA ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA YA UWAZI KUDHIBITI MIANYA YA RUSHWA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifungua kikao cha kuwasiliza wafanyabiashara na kupokea maoni yao juu ya sera,sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji kodi kwa mkoa wa Tanga kilicho hudhuriwa na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kushoto kulia ni Kamishna Msaidizi wa Forodha wa  TRA  kutoka makao makuu Benard Asubisye 
 Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo akizungumza wakati wa kikao hicho
 KAMISHNA Msaidizi wa Kodi za Ndani kutoka Makao Makuu Abdul Mapembe akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
 KAMISHNA wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA kutoka Makao Makuu Ben Asubisye akizungumza wakati wa kikao hicho kulia kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 MMOJA wa wafanyabiashara akichangia kwenye kikao hicho

 Sehemu ya wadau wa kikao hicho wakifuatilia matukio mbalimbali
 Sehemu ya wadau wakifuatilia kikao hicho
 Sehemu ya wadau wa kikao hicho wakifuatilia matumio mbalimbali
 Sehemu ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho
 Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Joseph Ngoyo kushoto akiwa na Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga wakifuatilia matukio mbalimbali
 SEHEMU ya wafanyabiashara na wadau wakiwa kwenye kikao hicho
MKURUGENZI wa kampuni ya Katani Limited Juma Shamte akichangia kwenye kikao hicho

NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo amesema kwamba mamlaka hiyo itaendelea na utekelezaji wa mikakati  ya kuhakikisha wanakuwa na mazingira ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji wa watumishi wao itakayojumuisha pamoja na kuzibiti mianya ya rushwa kupitia mifumo ya Tehama. 

Mbibo aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha kuwasikiliza wafanyabiashara na kupokea maoni yao juu ya sera,sheria ,kanuni na taratibu za ukusanyaji wa kodi kwa mkoa wa Tanga ikiwemo kuziangalia changamoto zinazowakabili ambapo alisema katika suala hilo wafanyabiashara wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kuhakikisha vitendo vya namna hiyo vinakomeshwa.

“Wafanyabiashara tunaomba ushirikiano wenu lakini pia niwaambie kwamba kwenye suala la uadilifu ni muhimu katika utendaji wa shughuli zenu za kila siku na hatutakuwa tayari kuona watumishi wanajihusisha na vitendo vya rushwa na kunyamaza tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi yao “Alisema 

Alisema wataendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuhakikisha wanakuwa na mazingira ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi kwa watumishi wao  kwa kuchukua hatua za haraka na nidhamu kwa watumishi wasio waaminifu huku akiwataka wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kuwafichua watumishi wanaohusika na vitendo vya rushwa miongoni mwa wale wasio waaminifu 

Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kuhakikisha wana kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya nchi yao kwa kulipa kodi kwani kodi hiyo inayopatikana kutokana na shughuli za kiuchumia ambazo zinafaywa na raia wa nchi hii. 

“Lakini sisi tutaendelea kuchukua juhuidi za makusudi kuhakikisha mfumo wa ulipaji kodi unakuwa rahisi utakaowezesha wafanyabiashara kuweza kuendesha biashara zake bila wasiwasi na kuweza kuzianisha na kuweza kuzitafutia ufumbuzi”Alisema Naibu Kamishna huyo wa TRA. 

Hata hivyo aliwaeleza wafanyabiashara mambo machache ambayo ni muhimu kuweza kupewa uzito ni utunzaji wa kumbukumbu sahihi za biashara ambalo ni jambo muhimu kwa ukuaji wa biashara muhimu kwa TRA na mfanyabiashara. 

“Lakini pia ni muhimu kwa vyombo vyengine ikiwemo vya fedha kwani zitasaidia uzibiti wa matumizi ya biashara pia kusaidia ukokotoaji sahihi hivyo kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima yanayoweza kujitokeza kati ya mlipa kodi na taasisi inayosimamia ulipaji wa kodi”Alisema 

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alimshukuru Naibu Kamishna huyo wa TRA kwa kufika mkoani humo kukutana na wafanyabiashara ambao ni uamuzi wa hekima,busara na ushirikiano . 

Alisema ushirikiano huo ulipelekea mwaka jana makusanyo kwa mkoa huo yalikuwa sio chini ya asilimia 80 lakini mwaka huu tumefikia si chini ya asilimia 91 hivyo tutaendelea kushirikiana kuziba mianya ya upotevu mapato ikiwemo uletaji bidhaa za magendo. 

“Magendo ni tatizo kubwa sana sio tu kwa wafanyabiashara miongoni mwenu mpo mnafuata sheria lakini baadhi yenu mnapitia nyia za panya kuleta magendo na kuuza bei ya chini na wanaofuata utaratibu wanaumia hivyo mapambano dhidi ya magendo yanaendelea hivyo nashukuru kwa ushirikiano huo tumepunguza shehena ya mzigo ambao ilikuwa inakamtwa kila mara “Alisema 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.