Na.Mwanajuma Juma. Zanzibar.
MWENYEKITI wa Chama Cha Soka
Zanzibar ZFF Wilaya ya Mjini Hassan Haji
Hamza ‘Chura’ amevitaka vilabu vya soka
nchini kufata utaratibu uliowekwa katika
kuendesha timu
zao ili kujiepusha na usumbufu wa kikatiba
na kianuni.
Akizungumza katika hafla ya ufungaji wa
mafunzo ya waalimu wa makipa wa mpira
wa miguu mwishoni mwa wiki iliyopita
alisema kuwa vilabu katika miaka hii
wasitarajie mteremko kutokana na uongozi
uliopo kuonesha kutaka mabadiliko katika
kila kona ya
mchezo huo.
Alisema kuwa uongozi huo mpya wameanza na kutoa mafunzo kwa waalimu wa makipa
hatua ambayo inaonekana itaendelea kwa kada zote zinazohusu soka.
“Napenda kusema kuwa inaonekana sasa Zanzibar inabadilika na kuelekea kule ambapo
tunataka na kwa hatua hii karibuni baadhi ya vilabu vingi vitakufa kutokana na watu ambao
wamekuja kusimamia misingi na kanuni za soka”, alisema.
Hivyo alisema kuwa kwa wale ambao wamekuwa wakionekana kuongoza kimazoea
wataweza kukaa pembeni kutokana na kuja kuona kwamba wanaonewa pale ambapo
watatakiwa wafate taratibu.
Aidha alifahamisha kwamba taaluma ni muhimu sana kwa sababu vilabu vingi
vimekuwa wakiwaacha nyuma makipa kutokana na kile alichodai kukosa wasimamizi.
Hivyo alisema kuwa kufatia hatua hiyo itawafanya na wao waweze
kutambulika na kupatiwa waalimu wa kuwafundisha ambao wataweza kuwatoa makosa yao
pale wanapokosea kama ambavyo ilivyo kwa wachezaji wengine.
No comments:
Post a Comment