Habari za Punde

Watahiniwa wa Kidatu Cha Sita Mwaka Huu Wamefaulu Vizuri Mitihani Yao 2019.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania Dkt. Charles E. Msonde, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, akitowa matokea ya Mitihani ya Taifa ya Kidatu cha Sita kwa mwaka huu, Mei 2019, katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Zanzibar.

Na.Mwanajuma Juma. Zanzibar.
JUMLA ya wanafunzi wapatao 88,069 wamefaulu mitihani yao ya kidato cha sita ikiwa ni sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mitihani.
Matokeo ya mitihani hayo yalitangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani 
Tanzania Dkt. Charles Enock Msonde mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa 
ufaulu wa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.74.
Alisema kuwa kati ya wanafunzi hao waliofaulu wasichana ni 37,219 sawa na asilimia 
99.11 na wavulana ni 50,581 sawa na asilimia 97.75 .
Aidha alisema kuwa katika matokeo hayo watahiniwa wa shule waliofaulu ni 78,666 
sawa na asilimia 99.14 ya waliofanya mitihani na watahiniwa wa kujitegemea ni 9,403 ikiwa 
ni sawa na asilimia 91.95 .
Alifahamisha kwamba juma la wanafunzi 91,298 walisajiliwa kufanya mtihani huo 
wakiwemo wasichana 37,948  sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na 
asilimia 58.44 ambapo watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani  na 
watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani kutokana na sababu 
mbali mbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.
Aidha alieleza kuwa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa 
wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 76,655 sawa 
na asilimia 96.61 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 
32,887 sawa na asilimia 97.22 na wavulana 43,768 sawa na asilimia 96.15.
Hata hivyo alisema kuwa takwimu za ufaulu kwa watahiniwa wa shule wa mwaka huu, 
ikilinganishwa na mwaka jana zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo ya Geography, 
Kiswahili, Engilish Language, French Language, Kiarabu, Basic Applied Mathematics, 
Advance Mathematics, Economics na Food anda Human Nutrition umepanda 
ikilinganishwa na mwaka jana.
Aidha alisema kuwa ufaulu katika masomo ya General Studies, History, Biology na 
Acountance umeshuka kidogo ikilinganishwa na mwaka 2018 .
Aidha Baraza ka Mitihani limefuta matokeo yote ya watahiniwa 14 waliobainika kufanya 
udanganyifu katika mitihani yao kati ya hao tisa ni watahiniwa wa shule na watano ni 
watahiniwa wa kujetegemea.

SHULE 10 BORA KITAIFA
Kisimiri ya Arusha, Feza Boys Dar Es Salaam, Ahmes ya Pwani, Mwandet ya Arusha, 
Tabora Boys Tabora, Kibaha Pwani, Feza Girls ya Dar Es Salaam, ST.Mary’s Mazinde 
Juu, Canossa ya Dar Es Salaam na Kemebos  ya Kagera.

SHULE 10 ZA MWISHO KITAIFA
Nyamunga ya Mara, Haile Selassie mjini Magharibi, Tumekuja Mjini Magharibi, Bumangi  ya Mara, Buturi ya Mara, Mpendae Mjini Magharibi, Eckernforde Tanga, Nsimbo Katavi, 
Mondo ya Dodoma na Kiembesamaki A Islamic ya Mjini Magharibi.

WATAHINIWA  10 BORA  KITAIFA KWA MASOMO YA SAYANSI
Faith Nicholous Matee (ST. Mary’s Mzinde Juu Tanga), Herman Pauline Kamugisha (Kisimiri Arusha),
Levina Calist Chami (ST. Coreti ya Kilimanjaro), 

Benius Eustace (Mzumbe ya Morogoro), 

Augostino Issaya Omari (Ilboru ya Arusha), 

Satrumin Arbogast  Shirima (Temeke Dar Es Salaam), 
Khalid Hussein Abdalla,  (Feza Boys Dar Es Salaam), 
Assad Y.Msangi  (Feza Boys Dar Es Salaam), 
Peter Jovenal Riima (Kibaha Pwani) na 
Augustine J. Kamba (Feza Boys ya Dar E Salaam).    

WASICHANA 10 BORA MASOMO YA SAYANSI
Faith Nicholous Matee (ST. Mary’s Mzinde Juu Tanga), Levina Calist Chami (ST. Coreti ya Kilimanjaro), 
Wahida Janguo (Feza Girls Dar Es Salaam), 
Vanessa R. Rutabana (Tabora Girls ya Tabora), 
Pielina M. Figowole (Tabora Girls ya Tabora), 
Loveness Samson Mloge (ST. Mary’s Mzinde Juu), Wahida Mbaraka Uzia (Zanzibar Feza Mjini Magharibi), Beatrice Martin Mwella (St. Mary’s Mzinde Juu), 
Consolata Seraphin Matee (St. Mary’s Mzinde Juu) na Maimuna A. Mshana (Marian Girls ya Pwani).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA MASOMO YA SAYANSI
Herman Pauline Kamugisha (Kisimiri Arusha), Benius Eustace (Mzumbe ya Morogoro), Augostino Issaya Omari (Ilboru ya Arusha), Satrumin Arbogast Shirima (Temeke Dar Es 
Salaam), Khalid Hussein Abdalla,  (Feza Boys Dar Es Salaam), Assad Y.Msangi  (Feza Boys 
Dar Es Salaam), Peter Jovenal Riima (Kibaha Pwani) na Augustine J. Kamba (Feza Boys ya 
Dar E Salaam).Shedrack Leonartus Siame (UWATA Mbeya) na Noel Godwin Maro (ST. 
Mary Goreti Kilimanjaro).

WATAHINIWA 10 BORA KITAIFA LUGHA NA SANAA
Victor Mtui (Feza Boys Dar), Paula  Nelson Lujwanga na Blandina Kessy Nyange (St. Mary Mzinde Juu Tanga), Eva J. Shitindi (Machame Girls Kilimanjaro), Ruhinda Benedicto 
Machimu (St. Mary Mzinde Juu Tanga), Anita Zacharia Massawe (ST. Mary’s Mzinde Juu 
Tanga), Karrim Kassimu Muhibu (Nyangao Lindi), Anold Andrea Msuya (Dareda Manyara), Latifa Mohammed Mrosso (Ahmes Pwani) na Elibariki Desidery Baliyanga (Lukole Kagera).

WASICHANA 10 BORA KITAIFA LUGHA NA SANAA
Paula Nelson Lujwangana, Blandina Kessy Nyange (St. Mary Mzinde Juu Tanga), Eva J. Shitindi (Machame Girls Kilimanjaro), Anita Zacharia Masawe (St. Mary Mzinde 
uu Tanga), Latifa Mohammed Mrosso (Ahmes Pwani), Mwanakombo Yussuf Ramadhan 
(Mtwara Girls Mtwara), Katarina Damas Shao (Kisimiri Arusha), Pakusana Henry Chaula (St. Mary’s Mzinde Juu Tanga), Minnah K. Mtingwa (Feza Girls Dar) na Jasintha 
Deogratias (Lukole Kagera).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA MASOMO YA LUGHA NA SANAA
Victor Mtui (Feza Boys Dar), Rushinda Benedicto Machimu (St. Mary Mzinde Juu Tanga), Karrim Kassimu Muhibu (Nyangao Lindi), Elibariki Desidery Baliyanga (Lukole Kagera). 
Joseph Anold Andrea Msuya (Dareda Manyara), Joseph Kelvin Komba (Kisimiri Arusha), 
Malugu M. Maganyala (Feza Boys Dar), Daudi Mbukwa (Kisimiri Arusha), Frank J. 
Mwampembe  na Paschal K. Nhumba (Lukole Kagera).

WATAHINIWA 10 BORA KITAIFA BIASAHARA
Noreen M. Lyimo (Baobab Pwani), Aston Stevin Ngaeje (Kibaha Pwani), Doreen A. Lipamba (Benjamin Willium Mkapa Dar), Emmanuel P. Chila (Alpha Dar), Mery D. Samwel  na 
Glory Danny Kandonga (Weruweru Kilimanjaro), Merciana A. Msechu (Mpanda Girls 
Katavi), Getruda  Didoris Ndongo (ST. Christina  Girls Tanga) na Athumani Magadura 
Willium (Umbwe Kilimanjaro).
WASICHANA 10 BORA KITAIFA BIASHARA
Noreen M. Lyimo (Baobab Pwani), Doreen A. Lipamba (Benjamin Willium Mkapa Dar), Mery D. Samwel  na Glory Danny 
Kandonga (Weruweru Kilimanjaro), Merciana A. Msechu (Mpanda Girls Katavi), 
Getruda Didoris Ndongo (ST. Christina  Girls Tanga), Irene Ishael Barakaeli (Nganza 
Mwanza), Rahel P. Kyokola (St. Mary Goreti Kilimanjaro), Salma A. Shekimweri (Kibasila 
Dar) na Grace Hayrod Ng’ondya (Weruweru Kilimanjaro).
WAVULANA 10 BORA KITAIFA BIASHARA
Aston Stevin Ngaeje (Kibaha Pwani), Gift Mwakikusi (Tusiime Dar), Emmanuel P. Chila (Alpha Dar), Athumani Magadura Willium (Umbwe Kilimanjaro), Stephano Y. 
Dismas (Kibaha Pwani), Robert John Tano (Scolastica Kilimanjaro), Dotee A. Zuberi 
Galanos Tanga), Ernest P. Game (Kibaha Pwani) na Deogratias Ladislaus Msilanga 
(Kibaha Pwani).
Hata hivyo alisema kuwa ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa na idadi ya 
watahiniwa waliofaulu vizuri katika daraja la kwanza  hadi la tatu imeongezeka kwa 
asilimia 1.09kutoka asilimia 95.52 ya mwaka 2018 na kuwa asilimia 96.61 ya mwaka 2019.
Aidha alisema kuwa ubora wa ufaulu wa wasichana kwa mwaka 2019 umezidi ule wa 
wavulana kwa asilimia 1.07.Sambamba na hayo alisema kuwa Baraza la Mitihani Tanzania 
lilifanya uchambuzi wa kina wa matokeo hayo kwa kila somo na kutoa machapisho ya 
uchambuzi huo yakatakayowasilishwa kwa wadau wa elimu zikiwemo shule zote za 
Sekondari za Juu (‘A’ Level) nchini kwa lengo la kuwezesha walimu kutumia taarifa za 
uchambuzi katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Hata hivyo katika matokeo hayo watahiniwa 20 wa shule ambao walipata matatizo ya 
kiafya na kushindwa kufanya mitihani kwa baadhi ya masomo yamezuiliwa matokeo 
hayo na watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani yao hiyo Mei mwakani 
kama watahiniwa wa shule.
Dkt. Msonde alisema kuwa Baraza linapenda kuchukuwa fursa hizo kuzipongeza kamati za 
Uwendeshaji Mitihani za mikoa na Halmashauri /Manispaa//Majiji nchini, Wakuu 
wa shule na wasimamizi wa mitihani kwa kuzingatia na kusimamia taratibu 
za uwendeshaji mitihani na hivyo kuzuia kwa kiasi kikubwa udanganyifu kufanyika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.