Habari za Punde

Waziri Mkuu afungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wakati alipotembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson, baada kutembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei). Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus Boisei. Tokea kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabula. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati  akifungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei).






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.