Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Rwanda Nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania inajivunia kufanya kazi kwa karibu na Nchi ya Rwanda kutokana na ukarimu mkubwa uliojengeka  kwa muda sasa kwa Wananchi wa Nchi mbili hizo.
Makamu wa Rais amesema hayo leo alipokutana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe.Eugene Kayihura wakati Balozi Kayihura alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais Baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuhakikishia Balozi Kayihura kwamba Tanzania itaendelea kudumisha Uhusiano wa Nchi mbili hizi uliodumu kwa muda mrefu sasa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kijamii hasa katika kuangalia fursa za kiuchumi pamoja na kuwa na uhusiano mzuri wa huduma ya Fedha kati ya Rwanda na Tanzania.
Mhe. Samia amesema muda umefika sasa kushirikiana pamoja kwa ajili ya kujenga Uchumi wa Mataifa haya, ambapo pia amempongeza Balozi Eugene Kayihura kwa Ushirikiano Mkubwa alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi chake chote cha kazi hapa Nchini na kumtakia kila la Heri kokote aendako katika kituo chake kipya cha kazi.
Nae Nalozi Eugene Kayihura amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba, Rwanda itaendelea kukuza na kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika pande zote za kimaendeleo na kuitakia Serikali ya Tanzania maandalizi mema ya mkutano wa SADC.
IMETOLEWA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.