Habari za Punde

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Yatoa Mafunzo ya Mkataba wa Huduma Kwa Wateja

Washiriki wakimsikiliza Afisa TEHAMA Mwandamizi Mkuu,Kitengo cha Kudhibiti Ubora wa Huduma Abibu  Rashid  wakati alipokuwa akitoa Mafunzo katika Ukumbi wa Polisi Madungu Kisiwani Pemba.
Na Miza Othman –Maelezo Pemba.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imehusisha muundo wake kuitikia wito wa kuiboresha utendaji ili kuwahudumia wananchi  vizuri zaidi.
Afisa TEHAMA Mwandamizi Mkuu, Kitengo cha Kudhibiti Ubora wa Huduma Abibu Rashid Ntahigiye ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa mafunzo kwa washiriki waliyofika katika Ukumbi wa Polisi Mdungu.
Sambamba na hayo ameleza kuwa uhusishaji wa muundo huo umeanza utekelezaji wa mfumo wa utoaji huduma  bora kwa kuzingatia kiwango kipya cha kimataifa chenye kuboresha huduma zao.
Afisa TEHAMA Abibu Rashid amesema (TCRA) imeandaa mkataba wa huduma kwa mteja kwa lengo la kutekeleza majukumu yake kwa uwazi ili kutimiza dhana ya uwajibikaji katika kazi yao.
Hata hivyo amesisitiza kusema madhumuni ya mkataba huo  ni kubainisha viwango vya kutoa huduma kwa wateja na kuuwarifu umma kuhusu TCRA ikiwemo kuzingatia viwango vya wateja wao.
Nae Mkuu wa Ofisi (TCRA) Zanzibar Esuvatie-Asisa Masinga amesema wanahitaji kukuza uhusiano kati ya watumishi na wateja ili kutenda haki na wajibu wa mteja kuhusiana na huduma wanazozitoa kwa lengo la kukidhi matarajio ya wateja na wadau wao.
“uwazi na uwadilifu katika kazi zetu vitakuwa kinga muhimu dhidi ya malalamiko kwa wananchi kama vitendo au viashiria vya rushwa na taasisi yetu” alisema Esuvatie-Asisa.
Aidha amesisitiza kwa kusema (TCRA) inalengo la kuboresha taratibu na kanuni za ndani kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa habari kwa wadau wote kwani upatikanaji sahihi bila vikwazo utaongeza uwazi na uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.  
Ni Mkataba wa mwanzo wa kihistoria  tangu kuanzishwa katika Mmlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.