Na Hawa Ali, Zanzibar.
Ligi daraja la Kwanza Kanda ya Unguja inatarajia kuanza kutimua Vumbi jumaa tatu hii msimu mpya wa mwaka 2019-2020.
Jumla ya Michezo mitatu inatarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti ambapo Bweleo na Dula Boys watakipiga uwanja wa Mao A, wakati Miembeni na Kikwajuni watapepetana katika kiwanja cha Mao B, huku watembeza watalii wa Nungwi timu ya Mundu watajitupa uwanja wa Amaan wakiminyana na timu ya Uhamiaji.
Akizungumza na Gazeti hili Mkurugenzi wa Kamati ya Mashindano ya ZFF Ali Mohammed alisema ligi ya msimu huu itakuwa ya namna yake ikiwemo hata mabadiliko ya Viwanja vya kucheza.
Alisema msimu huu katika kuboresha ligi hiyo imeona ipo haja ya kutumia viwanja vilivyopo mji wa Zanzibar ikilinganishwa msimu iliyopita ambapo mechi nyingi zilikuwa zikichezwa katika viwanja vya mashamba hali iliyopelekea hata kuongeza kwa wimbi la kupigwa Waamuzi.
Alisema msimu huu ligi daraja Kanda kwa kuanzia vitatumika viwanja viwili tu ambavyo ni kiwanja cha Amaan na kiwanja cha Mao ze dong Ili kupunguza malalamiko yanayotolewa na Waamuzi ikiwemo kupigwa na viongozi wa vilabu na hata mashabiki pindi wanapochezesha katika viwanja ambavyo walidai havina ulinzi wa kutosha.
“Msimu huu tutaanza na viwanja viwili kwanza huku tukiangalia mpaka dilisha dogo kama tutaongea viwanja vingine au tutatumia hapo hapo Mau na Amaan na tayari tushawaita viongozi wa vilabu tumezungumza nao juu ya mabadiliko haya ya Viwanja na wao wameelewa"Alisema
Ligi hiyo inatarajia kushirikisha timu 13 ambazo ni Kikwajuni, Miembeni, Taifa ya Jang'ombe, Mwembe Makumbi City, Bweleo, Dula Boys, Mchangani United, Mundu, Kilimanicity, Uhamiaji, Idumu, na Blak sailor
No comments:
Post a Comment