Habari za Punde

Maandalizi ya Uzinduzi wa Mpango wa Kutokomeza Kipindupindu Zanzibar Yakamilikia.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed, akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusina na Uzinduzi wa Mpango wa Kutokomeza Kipindupindu Zanzibar, katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Zanzibar.

Na. Bahati Habibu  Maelezo.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa , UNICEF, KOICA na wadau wengine imekusudia kutokomeza maradhi ya kipindupindu ifikapo mwaka 2028 kisiwepo tena nchini.
Hayo ameyasema leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mpango wa kutokomeza kipindupindu  katika ukumbi wa Wizara ya Afya uliopo Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Amesema Serikali imefanikiwa kudhibiti maradhi ya kipindupindu kupitia jitihada ikiwa ni pamoja na kueka sheria na kanuni za afya, kuimarisha miondominu ya afya na mazingira na kuimarisha miondombinu ya maji na kuongeza upatikanaji wa maji safi ya mifereji.
Aidha amewataka waandishi wa habari kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kila mwananchi aweze kuwa na elimu ya kutokomeza kipindupindu na maradhi mengine ya kuharisha kwa kupitia vyombo vya habari.
Nae Mkurugenzi mtendaji kamisheni maafa Zanzibar Makame khatib Makame  amesema katika kuhakikisha mpango huu unatekelezwa ipasavyo umeshirikisha taasisi  zisizopungua nane.
Pia Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil M. Abdalla amesema mpango huo wa kutokomeza kipindupindu utagharimu jumla ya dola milioni 51 za kimarekani  katika kipindi cha miaka kumi.
Mpango wa kutokomeza maradhi ya kipindupindu ,ugonjwa wa kuharisha na magonjwa mengine unatarajiwa kuzinduliwa siku ya jummane ya taarehe 10 mwezi huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohamed Abdalla, akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari juu ya  Uzinduzi wa Mpango wa Kutokomeza Kipindupindu Zanzibar  Ukumbi wa Wizara ya Afya Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Sabra Issa Machano, akiongoza ziara  kwa Waziri wa Fedha na Mipango, alipotembelea Kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo  Zanzibar.
Picha na Abdalla Omar 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.