Habari za Punde

Mabingwa Kombe la Mabingwa wa Muungano Ndondo Cup Timu ya Theo Kombaini ya Zanzibar.

Wachezaji wa Timu ya Ndondo ya Theo Kombaini wakishangilia Ubingwa wao baada ya mchezo wao wa Fainali ya Ndondo Cup Muungano kumalizika kwa kuwafunga Timu ya UV Temeke kutoka Jijini Dar es Salaam baada ya kuifunga katika mchezo wa Fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Theo wametangazwa Mabingwa wa Ndondo Muungano kwa mwaka 2019 /2020.
Wachezaji wa Timu ya UV Temeke wakiwa na simazi baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 dhidi ya Timu ya Theo Kombaini katika mchezo wa Fainali ya Mabingwa wa Ndondo wa Zanzibar na Dar es Salaam, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Viongozi wa Mpira Jijini Dar esc Salaam wakiwa na majonzi baada ya Timu yao ya UV Temeke kukubali kipigo cha bao 3-1, dhidi ya Timu ya Theo Kombani ya Zanzibar mchezo uliofanyikia Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi Chti Mchezaji wa Theo Kombani Ramadhani Manyama kwa kushiriki Michuano ya Ndondo Coconut kwa mara Nne bila kukosa na kujiuzulu rasmin kushiriki michuano ya ndondo Zanzibar.
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira Zanzibar ZFF Ndg. Seif Kombe Boss akimkabidhi zawadi Mchezaji Bora wa Fainali ya Ndondo Cup Hassan Haji, kwa kuonesha kiwango cha mpira wakati wa mcheszo huo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu yake imeshinda kwa bao 3-1. 
Kiongozi wa Chama Cha Mpira Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Kasongo akimkabidhi zawadi Ngao na Kitita cha Fedha mshindi wa Pili wa Kombe la Ndondo Muungano Nahodha wa Timu ya UV Temeke Hans Mgaya, baada ya kumalizika mchezo huo wa Fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Theo Kombani imeibuka Bingwa wa Muungano Ndondo Cup, kwa mwaka 2019/2020.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi Kitita cha Fedha na Ngao Nahodha wa Timu ya Theo Kombaini Ramadhani Manyama, baada ya Timu yake kuibuka Mabingwa wa Muunganoi Ndondo Cup, kwa mwaka 2019/2020. 
Mwanamichezo na Kiongozi wa Mpira Jijini Dar esc Salaam Shafi Dauda akimkabidhi zawadi Kipa Bora wa Fainali ya Kombe la Muungano Ndondo Cup Kipa wa Timu ya Theo Kombaini Ali Othman.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.