Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi.Seif Ali Iddi Atembelea Ebeo la Ujenzi wa Mji wa Kisasa Kwahani Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akifanya ziara ya kutembelea eneo linalotaka kujengwa Mji Mpya wa Mtaa wa Kwahani Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Hassan Khatib Hassan wa kwanza kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bibi Marina Joel Thomas wakiangalia eneo lilosafishwa kwa ajili ya kuanza Mradi wa Nyumba za Kisasa Mtaa wa Kwahani.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Iddi Haji Makame akimpatia maelezo Balozi Seif jinsi mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa utakavyofanyika katika Mtaa wa Kwahani.
  Balozi Seif akiwapongeza Wananchi wa Kwahani kwa Uzalendo wao wa kupisha Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa ambazo utawafaidisha na wao mara zitakapokamilika ujenzi wake.
 Mkurugenzi Uwekezaji na Utafiti wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF} Nd. Abdulatif Ibrahim Iddi akitoa taarifa ya hatua za mwanzo zilizochukuliwa na maandalizi ya kuanza kwa Mradi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.