Habari za Punde

Malindi yashindwa kutamba nyumbani kombe la shirikisho yafungwa 4-1 n a timu ya Al Masry kutoka Misri

Na Mwajuma Juma
WAWAKILISHI wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Malindi wameshindwa kutamba nyumbani kwao mbele ya Almisry kwa kukubali kichapo cha mabao 4-1

Mchezo huo wa awali ulichezwa kwenye uwanja wa Amaan saa 10 za jioni na kutoa ushindani mkali kwa wapinzani wao ambao walionekana kuwazidi kwa kila Idara timu ya Malindi.

 Almisry mabao yake mawili yalifungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27 na 39 , Hassan Ibrahim dakika ya 33 Saidou Simpore dakika ya 52 na Malindi lilifungwa na Ibrahim Ali 'Imu Mkoko ' dakika ya 42.


Timu hizo zitarejeana Tena Septemba 29 mwaka huu, mchezo ambao utapigwa nchini misry pasipo na mashabiki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.