Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Uhalifu Khamis Mwinyi Bakari akijibu maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari katika hafla ya utoaji wa Takwimu za makosa ya Barabarani ambapo imeonesha kuongezeka kutoka ajali 20 kwa mwezi wa Septemba 2018 hadi ajali 27 mwezi wa Septemba 2019 sawa na Asilimia 35 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali Zanzibar.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kitengo cha Takwimu za Makosa ya Jinai,Madai na Jinsia Asha Mussa Mahfudha (katikati) akitoa Takwimu za makosa ya Barabarani ambapo imeonesha kuongezeka kutoka ajali 20 kwa mwezi wa Septemba 2018 hadi ajali 27 mwezi wa Septemba 2019 sawa na Asilimia 35 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali Zanzibar.
Muandishi wa Habari wa ITV Farouk Karim akiuliza maswali atika hafla ya utoaji wa Takwimu za makosa ya Barabarani ambapo imeonesha kuongezeka kutoka ajali 20 kwa mwezi wa Septemba 2018 hadi ajali 27 mwezi wa Septemba 2019 sawa na Asilimia 35 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.
Na. Mwashungi Tahir Maelezo 15-10-2019.
Jumla ya makosa ya barabarani 1,853 yameripotiwa mwezi wa Septemba 2019 kupungua ambapo Septemba 2018 yalikuwa 2,741 sawa na asilimia 12.6.
Akitoa taarifa Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu ya Serikali kitengo cha Takwimu za Makosa ya Jinai Madai na Jinsia Asha Mussa Mahfoudh wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kuhusu makosa ya barabarani.
Amesema miongoni mwa makosa hayo ni pamoja na kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani , kuzidisha idadi ya watu na mizigo, kuendesha chombo cha moto gari, vespa, pikipiki/fifti bila ya leseni , bima na leseni ya njia.
Pia amesema Wilaya ya Magharibi B ina idadi kubwa ya makosa ya barabarani 345 sawa na asilimia 18.6 kati ya makosa yote yaliyoripotiwa, na upande wa Wilaya ya Kusini ina idadi ndogo ya makosa ya barabarani yaliyoripotiwa ni 35 sawa na asilimia 1.9.
Kwa Upande wa ajali za barabarani amesema jumla ya ajali 27 zimeripotiwa mwezi wa Septemba , 2019, waathirika 58 ambao kati ya hao 45 walikuwa ni wanaume sawa na asilimia 77.6 na wanawake 13 sawa na asilimia 22.4 miongoni mwao waliokufa ni 17 sawa na asilimia 29.3 na waliojeruhiwa 41.
Amesema Wilaya ya Mjini imeripotiwa kuwa na ajali nyingi ambazo nane , zikifuatiwa na Wilaya ya Magharibi A, Wete na Chake Chake zikiwa na ajali nne kwa kila mmoja,Wilaya ya Wete imeripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya walioathirika ambao ni 17, sawa na asilimia29.3.
Wanaoathirika katika ajali za barabarani ni pamoja na wanaotembea kwa miguu, wapanda baskeli , pikipiki, , madereva na abiria.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za uhalifu Zanzibar pia ni mkaguzi wa Jeshi la Polisi Khamis Mwinyi Bakari amesema elimu inahitajika zaidi kwa madereva juu ya kufuata sheria za barabarani.
Amesema ongezeko za ajali pamoja na vifo zinasababishwa na madereva kuwa wazembe, kuendesha gari mwendo wa kasi na kila mmoja kujiamuliya mwenyewe anavyotaka pasi kufuata sheria zilizowekwa .
Hivyo amewaomba madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika kwani jamii nayo inahitaji amani katika safari zao.
No comments:
Post a Comment