Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Amefanya Uteuzi wa Viongozi Katika Taasisi za Serikali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Viongozi katika Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo na Taasisi zao.

Bwana.Abdalla Rashid Abdalla ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa.

Bwana. Ali Mzee Ali  ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Historia na Mambo ya Kale.

Bwana Mwalim Ali Mwalim ameteuliwa kuwa Mshauri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati. 

Uteuzi huo umeaza jana 30,septemba 2019 .

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.