Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Amuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli Kuhudhuroa Kuapishwa Kwa Rais Mpya wa Botswana

Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Edgar Lungu wa Zambia kwenye Hafla ya kuapishwa Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi  iliyofanyika leo Novemba 01, 2019 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana.
Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Edgar Lungu wa Zambia na Rais Emmason Mnangagwa wa Zimbabwe wakishuhudia wakati Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi  alipokuwa akila kiapo kuiongoza Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena  Jijini Gaborone Botswana
Rais Mpya wa Botswana Dkt.  Mokgweetsi E. K. Masisi  akihutubia Viongozi wa Nchi mbalimbali na Wananchi wa Botswana Baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena  Jijini Gaborone Botswana.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.