Habari za Punde

UZINDUZI WA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA VICHWA VIKUBWA NA MIGONGO WAZI


  Naibu Waziri wa Afya Harous Said Suleiman akifungua pazia la Uzinduzi wa Ofisi ya Umoja wa wenye Vichwa vikubwa na Migongo wazi huko Fuoni Moroko.

Na Ali Issa na Suhaila Pongwa Maelezo          28-11-2019
Waziri wa Afya  Hamad Rashid Mohamed  amewataka akinababa kuacha kuwatelekeza wake zao pale ambapo wanapojifungua watoto wenye ulemavu na badala yake washirikiane  katika malezi ili  waweze kuwapatia  haki zao za msingi watoto hao.

Akizunguza kwa niaba yake leo Naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Said Suleiman wakati alipokuwa katika uzinduzi wa Ofisi ya umoja wa wenye vichwa vikubwa na migongo wazi huko Fuoni Moroko Wilaya ya Maghari B Unguja.
Amesme kuna baadhi ya kina Baba  huwa hawaoneshi ushirikiano pale ambapo wake zao wanapo jifunguwa watoto wenye ulemavu badala yake huchukua uwamuzi wa kuwapa talaka .
Madaktari wetu hupata shida ya kuwanyamazisha wakina mama pale ambapo wanapokuwa na masikitiko ya kupewa talaka kwa sababu ya kuzaa mtoto mlemavu ""alisema  Naibu Waziri.
Amefahamisha kuwa  watoto wenye  vichwa vikubwa na migongo wazi , wanahitaji kuoneshwa mapenzi  makubwa kutoka kwa wazee wao .
Aidha amewataka akina baba kuacha dhana potofu ya kuwa kuzaa mtoto mwenye ulemavu ni kupata nuksi katika familia  kwani hiyo ni rehema zake Mwenyezi Mungu.
 " kuna baadhi ya wazazi wana itikadi potofu mama anapo mzaa mtoto mlemavu mtoto mwenye ulemavu husema ni nuksi na kina baba huwaza njia za kuwatelekeza mama na mtoto ""alisema Naibu waziri.

Nae Katibu wa umoja huo Hussein Mohamed Saleh amewataka akina baba walio hudhuria kataika uzinduzi huo kuifikisha elimu  kwa wazee wenziwao ili kuweza kuacha kuwapa talaka kina mama kwa sababu ya kujifungua mtoto mlemavu .
Aidha amewapongeza Madaktari wandani na wanje kwa kuonesha ushirikano kwa kuwapatia matibabu watoto hao kwa kila pale panapo hitajika. 
Hata hivyo wimeiomba Serikali na wahisani mbali mbali kuwatatulia changamoto zinazo wakabili ikiwemo uhaba wa dawa , ukosefu wa eneo la ofisi ya kudumu , karakana ya ujasiriamali , usafiri na vitendea kazi vya ofisi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi 
Umoja wa wenye vichwa vikubwa na migongo wazi ulianzishwa tarehe 23-5-2018 ambapo ulikuwa na jumla ya wanachama 37.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.