Habari za Punde

KONGAMANO LA UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan akitoa maelezo kuhusu jinsi ya kulidhibiti suala la udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kongamano la Wasaidizi wa Sheria .(kulia) ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar(ZAFELA) Jamila Mahmoud .Muakilishi wa UNICEF kwa upande wa Zanzibar Joseph Magazi na Mjumbe wa Bodi  ZAFELA ,Fatma Gharibu huko katika Ukumbi wa Sanaa,  Rahaleo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar(ZAFELA) Jamila Mahmoud akifahamisha jinsi ya kesi za udhalilishaji zinavyozidi kukidhiri siku hadi siku huko katika kongamano la Wasaidizi wa Sheria .kulia ni Muakilishi wa UNICEF kwa upande wa Zanzibar Joseph Magazi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria  kutoka Wilaya ya Magharibi B Wilaya ya Kati na Kusini pamoja na Madiwani  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Hassan Khatib Hassan (hayupo pichani )huko katika kongamano la kupinga vitendo vya udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar .
Picha na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar .
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan ameitaka jamii kubadilika katika mfumo mzima wa makuzi na  malezi ili kuweza kuwasaidia watoto kuepukana na vitendo vya udhalilishaji .
Hayo ameyasema wakati alipofungua kongamano la Wasaidizi wa Sheria lenye lengo la kupiga vita udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto huko katika ukumbi wa Rahaleo Zanzibar
Alisema jamii iwe tayari kuanzisha  mbinu shirikishi katia malezi na makuzi ya  watoto wao kwa kuwa na uwezo wa kuwafatilia nyendo zao kwa wakati wote ili kuwaepusha na vitendo hivyo
Aidha alisema Malezi yaliyopo hivi sasa yemeweza kubadilisha Mila Silka na Tamaduni za Kizanzibar jambo ambalo linachangia udhalilishaji .
‘Iwapo Mzazi au mlezi anampeleka Mtoto mdogo  katika Sherehe za Harusi jambo hili ni kinyume na maadili yetu tuliyoyazowea na inachangia vishawishi  ,”alisema Mkuu huyo.
Alifahamisha kuwa utandawazi umeiharibu jamii kwa kuutumia vibaya hivyo iko haja ya kukaa na watoto kuwapa mafunzo mema katika maisha yao ya baadae  ili waweze kujielewa  .
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa wakati umefika sasa  kutizama chanzo cha tatizo la udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto pindipo ukijulikana chanzo chake unauwezo wa kutatuka  .
Nae Mkurungezi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Jamila Mohamoud  amewataka Wasaidizi wa Sheria kuisaidia jamii ili kuitetea haki ya mwanamke na mtoto kutokana na kukosa uelewa jambo linalochangia kutokuwa na imani na Mahakama
Alisema changamoto zilizopo katika jamii baba, babu, kaka, baba wa kambo na  mjomba kumdhalilisha mtoto mdogo  jambo ambalo ni unyama uliokidhiri ,katika kuhakikisha linaondolewa hili ni kusimamiwa  haki katika suala zima la udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto .
Kwa upande Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ramadhani Nasibu alisema rushwa bado imekidhiri katika ngazi zote jambo hilo linaikosesha jamii kuitete haki yao .
Alisema kuwa Mashahidi kushindwa kufika mahakamani kwa  kutoa ushahidi jambo hili huchangia kumkosesha haki mtendewa kosa la udhalilishaji .
Nao Washiriki wa kongamano hilo walisema bado elimu inahitajika kwa jamii ili kuweza kuisimamia haki isipotee
Hata hivyo wameeleza kuwa kutengana kwa wanandoa kunachangia kwa kiasi kikubwa vitendo vya udhalilishaji na  watoto kukosa malezi bora  jambo ambalo linawaumiza kisaikologia

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.