Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akitoa maagizo wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kutafuta kuandaa maandiko ya kuomba ufadhili wa mradi huo pamoja na kuandaa mpango mkakati wa kutekeleza programu hiyo leo Jijini Dar es Salaam, alipotembelea Ofisi za Mratibu wa Programu wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, (katikati) ni Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili.
Na Anitha Jonas –
WHUSM. Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi aagiza Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni na Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la
Afrika kuhakikisha wanarasimisha Programu ya Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika.
Dkt.Possi ametoa
agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Ofisi ya Mratibu wa
Programu ya Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika kwa lengo la kupata taarifa ya
utekelezaji wa Programu hiyo pamoja na kufahamu mpango wa kuiendesha.
“Kaeni pamoja na muandae Mpango Mkakati pamoja na Maandiko ya
kuomba Ufadhili wa Programu na mpango huo uwe unatoa dira ya namna Programu itatekelezwa sababu niyakimataifa na siyo wa Tanzania pekee kwani
kuna nchi za Afrika zinahusika na nchi za ulaya hivyo ni vyema kuwa na mpango
madhubuti wa utekelezaji wa Programu hii,”alisema Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza
Dkt.Possi alisistiza kuwa kwanza Mratibu wa Programu anapaswa kuwa na Kanzi
data ya Mawasiliano ya kila nchi iliyohusika katika harakati za ukombozi wa
Bara la Afrika kuanzia katika ngazi za Kitaifa mpaka Kimataifa na hii itarahisisha
utekelezaji wa shughuli za programu na usambazaji wa taarifa.
Pamoja na hayo nae
Kaimu Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
Bw.Christopher Mhongole alieleza kuwa programu inamalengo makuu manne ambayo
mojawapo ni Kuamsha Tafiti za Ukombozi wa Bara la Afrika,Kuenzi Mashujaa
waliyopigania Uhuru pamoja na Kuratibu Programu kwa kushirikiana na nchi
wanachama.
Aidha, Bw.Mhongole alieleza pia Programu hiyo
ilianza kuratibiwa na Wizara kuanzia mwaka 2011 na shughuli mbalimbali
zimefanyika ikiwemo ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wapigania uhuru wa
kitaifa pamoja na ukusanyaji wa nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikizungumzia
harakati ya ukombozi wa Bara la Afrika.
Halikadhalika nae
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili alikiri
kupokea melekezo ya Kaimu Katibu Mkuu huyo na kueleza kuwa Idara itakwenda
kuyafanyia kazi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akikagua hali ya Jengo ndani lilokuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika ambalo kwa sasa linafanyiwa ukarabati ili kuliongezea ubora na kuhifadhi historia yake alipotembelea Ofisi ya Mratibu wa Programu ya Ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam,(wa kwanza kushoto) Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
Afisa Utamaduni Bw.Christopher Mhongole anayemuwakilisha Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika (wa kwanza kulia) akimwonesha kwa nje Ukarabati unaondelea wa Jengo lilokuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara katika ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment