Habari za Punde

raza akabidhi vifaa vya michezo watoto mapinduzi cup

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akionyesha Kombe alilokabidhiwa na Mfanya biashara Mohammed Raza kutoka katika Kampuni ya (ZAT) kwa ajili ya Mashindano ya Mpira wa Miguu Zbc Watoto Mapinduzi Cup 2019-2020 hafla iliyofanyika Ukumbi wa Zbc.

Na Kijakazi Abdalla    Maelezo  
WAZIRI wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mahamuod Thabit Kombo ameishukuru Kampuni ya ZAT kwa kuonesha moyo wa uzalendo kwa kusaidia vifaa mbali mbali  vya michezo kwa ajili ya mashindano ya mpira wa miguu ZBC watoto  Mapinduzi CUP 2019-2020.
Akitoa pongezi hizo huko Shirika la Utangazaji  Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya  michezo na Kampuni  ya ZAT kwa ajili ya mashindano ya mpira wa miguu ZBC watoto Mapinduzi CUP 2019 -2020.
Amesema kuwa Kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kwa utoaji wa misaada kila  wanapotakiwa kutoa  jambo ambalo limekuwa likiwa linavutia zaidi katika michezo kwa watoto.
Pia  alisema kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikitumia uzalendo zaidi kwa nchi kwa kujali mapinduzi matukufu ya kumkomboa mzanzibar yaliyofanyika mwaka 1964 chini ya kiongozi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Vilevile Mheshimiwa Mahamuod amelishukuru  Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa kuandaa mashindano hayo na kuyataka yawe endelevu kila mara unafika wakati wake.
Aidha amewataka kutumia fursa  zaidi ya kuyatangaza mashindano hayo kwa makampuni mbalimbali ili ziweze kufadhili zaidi mashindano hayo kupitia kwa makampuni ya ndege ambayo yanakuja Zanzibar.
Nae Mwenyeki wa Kampuni ya ZAT Mohammed Raza Hassanal ameahidi kutoa misaada zaidi kila pale panahitajika kutoa misaada katika sekta zote ili kujenga nchi .
Aidha amezitaka kampuni kujitokeza kuchangia msaada kwa ajili ya mashindano hayo ila alissitiza zaidi misaada hiyo ifike kwa wkati na isiwe na masharti magumu.
Nae Naibu Mkurugenzi WA Shirika La Utangazaji Zanzibar Nassra Mohd  ameishukuru Kampuni ya ZAT kwa msaada huo na kuhakikisha kuutumia kwa lengo lililo kusudiwa.
Vifaa vilivyokabidhiwa kwa Mashindano ya mpira wa miguu ZBC Watoto Mapinduzi CUP 2019-2020 ni Kombe kwa ajili ya mshindi wa kwanza,kikombe kwa mshindi wa pili,kikombe kwa mshindi wa tatu,seti ya jezi 11,jezi ya goal keeper bora pamoja na gloves.jezi kwa mchezaji bora,viatu vya mpira kwa mfungaji bora,jezi na filimbi kwa muamuzi bora,medali 25 za dhahabu kwa mshindi wa kwanza,medali 25 za fedha kwa mshindi wa pili,medali  25 za shaba kwa mshindi wa tatu , seti ya jezi kwa mshindi wa kwanza na wapili pamoja na mipira 20.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.