Habari za Punde

Uzinduzi wa Barabara ya Bububu, Mahonda Hadi Mkokotoni Iliyojengwa Kwa Kiwango cha Lami,Ikiwa niu Shamrashamra za Kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifunua kipazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la Ufunguzi wa Barabara ya Bububu, Mahonda hadi Mkokotoni iliyojengwa kwa Kiwango cha lami, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akitowa maelezo ya mchoro wa barabara iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Bububu kwac Nyanya (Chuini) Mahonda hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, (kushoto) kwa Rais Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dkt. Sira Ubwa.  
Wananchi wa maeneo ya Bububu Chuini wakifuatilia ufunguzi wa Barabara ya Bububu, Mahonda hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa ufunguzi huo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) ufunguzi huo umefanyika kwa Nyanya (Chuini) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata uteke kuashiria kuifungua barabara ya Bububu hadi Mkokotoni iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Ujenzi kutoka Chini ya  (CCECC) (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe.Dkt, Sira Ubwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi  (CCECC) Kanda ya Afrika Mashariki Bw.Zhang Junle na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Meneja Mkaazi Bw.Alex,M.Mubiru
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Bububu,Mahonda hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais )Waziri wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Mhe.Dkt. Sira Ubwa na(kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibaer.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe. wakitembelea barabara hiyo baada ya ufunguzi wake. 
Wananchi wa maeneo ya Bububu Chuini wakifuatilia ufunguzi wa Barabara ya Bububu, Mahonda hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa ufunguzi huo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) ufunguzi huo umefanyika kwa Nyanya (Chuini) 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.