Habari za Punde

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Watembelea Miradi ya ZSSF na Kuridhishwa na Utekelezaji wa Miradi hiyo Zanzibar.

Meneja Mipango, Uwekezaji na Utafiti ZSSF Ndg. Abdulazizi Ibrahim, akitowa maelezo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wa Kamati ya Bajeti , wakitembelea mmoja wa Mradi wa ZSSF michezani Jijini Zanzibar kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Miradi ya Jengo la Kheikh Thabit Kombo na Michezani Mall. wakiwa katika ziara yao  
MSHAURI Muelekezi ujenzi wa nyumba za Kwahani, Andrian Eradius, akifahamisha jambo kwenye ramani, baada ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti Baraza la Wawakilishi kwenda kujionea ujenzi wa nyumba hizo unavyoendelea.
MWENYEKITI Kamati ya Bajet Baraza la Wawakilishi, Mohamed Said Dimwa, akiongoza kikao cha kamati hiyo kuzungumza na uwangozi wa Mfuko wa Hifadhi Jamii Zanzibar ZSSF, Kilimani Mjini Unguja.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Khamis Mussa, akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa nyumba za Kwahani, mbele ya Kamati ya Bajet Baraza la Wawakilishi, hafla iliofanyika ukumbi wa ZSSF Kilimani.
MKURUGENZI Muendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF, Sabra Issa Machano, akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa maduka ya Michezani Shoping Mall, mbele ya Kamati ya Bajet Baraza la Wawakilishi, hafla iliofanyika ukumbi wa ZSSF Kilimani.
WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti Baraza la Wawakilishi wakifuatilia ripoti za ujenzi wa Kwahani New City, na ujezni wa maduka ya Michezani  Shoping Mall.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.