Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusiana na Kuzuinya Mikusanyiko na Kufungu Skuli za Awali hadi Sekondari na Vyuo Vikuu Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar,kuhusiana na kubainika kwa mgonjwa wa maradhi ya Corona raia wa Ghana akitokea nchini ujerumani na kuwasili Nchini kwa Ndege ya Kenya Airway, 13/3/2020 saa tatu asubuhi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, mtu huyo ni mwanaume mwenye umri wa miaka 24, Mtu huyo akiwa amelazwa katika sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya maradhi ya mripuko huko katika eneo la kidimni Wilaya ya Kati Unguja. Kwa sasa anaendelea na matibabu hali yake inaendelea vizuri. (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na(kuli) Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma. taarifa hiyo imetolewa katika ukumbi wa Sheikh Idisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.  

Serikali imechukua hatu ya kuzifunga Skuli zote za Maandalizi,Msingi,Sekondari, Vyuo Vikuu pamoja na Madrasa ili kupunguza maambikizo ya maradhi hayo.

Pia amesema kuzuiya mikusanyiko yote inayokutanisha watu wengi kwa wakati mmoja, ikiwemo mikutano, makongamano,semina,warsha, michezo ya ligi kuu ligi za kanda pamoja na burudani za ngoma na shughuli za harusi mpaka hali ya maradhi hayo itakapotengemaa. 
Na kuhusu shughuli za maziko taarifa itatolewa na viongozi wa dini na taasisi husika. 

Serikali inakemea vikali utumiaji wa bandari zisizo rasmin kwa ajili ya kuchukua abiria na mizigo hivyo wato wote wanatakiwa kutumia bandari zilizo rasmin za malindi, mkokotoni kwa upande wa Unguja na Mkoani, Wete na Wesha kwa upande wa Pemba.Hata hivyo vyombo vitakavyotumika nje ya bandari zisozo rasmin vitataifishwa na Serikali.

Kama Mtu atakuwa na dalili za ugonjwa huu anatakiwa kubaki nyumbani na kutumia namba hizi za simu kuwasiliana na wahusika kwa hatua zaidi 

0777 454675 - 0777 948426 -0777461230 na 0777787749. 

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati akizungumza na wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar(hawapo pichani) akitowa taarifa ya kwa Umma kuhusiana na maradhi ya Corona Virusi katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati akizungumza na wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar akitowa taarifa ya kwa Umma kuhusiana na maradhi ya Corona Virusi katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.