Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe Zungu Afanya Ziara Wilayani Sengerema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akisikiliza taarifa ya msitu wa asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye ekari 12.3 kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Ndg.Salim Ali (kulia) alipofanya ziara wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Ndg.Joseph Kipolena wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Ndg. Magesa Mafuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia msitu wa asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye ekari 12.3 uliopo katika  eneo la Makao  Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambao unatumika kama shamba darasa kwa wananchi kuhusu uhifadhi endelevu wa misitu ya asili katika maeneo hayo ambao kwa mujibu wa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Sengerema Ndg.Salim Ali, utasaidia kunyonya hewa chafu, upatikanaji wa wa kuni kupitia uvunaji maalumu na uwekaji wa shughuli rafiki kwa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akipanda mti na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani wilayani Sengerema mkoani Mwanza alipofanya ziara ambapo pia alizungumza na wanafunzi wa shule hiyo kuhusu utunzaji mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitembelea na kukagua kikundi cha mazingira Bwawani wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambapo aliwapongeza na kuwatangaza kuwa mabalozi wa Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani ambapo aliwataka wawe mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira.
(Picha na  Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.